Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 14 March 2015

POLISI YAVAMIA OFISI ZA CUF, YAKAMATA VIONGOZI TISA


Na Mwandishi Wetu, Dar es SalaamCHAMA cha Wananchi (CUF) kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani Mtwara kuvamia ofisi za chama hicho na kuwakamata wanachama tisa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Naibu Mkurugenzi Habari na Uenezi wa CUF, Abdual Kambaya, ilisema Machi 12, mwaka huu kati ya saa saba mchana hadi saa 10 jioni, polisi walifika katika ofisi za chama hicho na kupekua bila kusema wanatafuta nini.
“Walipekua ofisi na baadaye walihamia katika nyumba za wanachama mbalimbali na kuendeleza upekuzi wao, leo hii (jana) wameendelea na kamatakamata yao na kumkamata Mwenyekiti wa CUF Wilaya, Salimu Mchumbila na Katibu wake, Saidi Kulagha ,” alisema Kambaya.
Alisema wanachama hao walichukuliwa na polisi na kupelekwa kusikojulikana.
“CUF Taifa tulipopata taarifa hiyo tulianza kufuatilia na RPC wa Mtwara alisema hana taarifa ya tukio hilo,” alisema Kambaya.
Alisema CUF kina taarifa za ndani kuwa baadhi ya wanasiasa mkoani humo wanahusika na ukamataji huo ili kudhoofisha chama hicho katika kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.
“CUF kama chama tunasema mchezo huu hautafanikiwa na tunawahidi na kuwahakikishia kuwa hawataweza, tunalaani kitendo hiki cha polisi kuendelea kutumiwa na CCM kuisaidia harakati zake,” alisema Kambaya.
Alisema kwa sasa chama hicho kinaendelea kufuatilia walipo vijana hao na baadaye watatoa tamko la hatua gani watachukua dhidi ya jambo hilo.
Aliwataja wanachama wengine waliokamatwa kuwa ni Mjumbe Mkutano Mkuu, Ismail Njalu, Mwenyekiti wa Vijana, Sadick Songoni, Katibu Kata Vijae, Ahmed Kisewe.
Wengine ni Mwenyekiti Uhamasishaji/Mjumbe wa Kamati Tendaji, Seleman Nandondende, Mjumbe wa Kamati Tendaji, Iron Lankila, Mkurugenzi wa BG, Yasin Okororo na Mjumbe Said Mtondo.
CREDIT: MTANZANIA

No comments:

Post a Comment