Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 14 March 2015

MUME ACHOMWA KWA KUMKUMBUKA MAREHEMU MKEWE


Mwanaume aliyechomwa na maji moto kwa kumkumbuka marehemu mke wake wake amesema kuwa haoni haya kamwe kwa kitendo alichofanyiwa na mpenzi wake.

Ken Gregory, 65, anayetokea Peterborough, Uingereza amesema kuwa wanaume wanaopondwa kuteswa ama hata kupigwa na wake wao hawapaswi kuona haya.
Yamkini Gregory alikuwa amepanga kutembelea kaburi la mke wake kwa sababu ilikuwa siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake lakini hoja hiyo ikapingwa na mke wake wakati huo Teresa Gilbertson, 60 .
Mume aliyechomkwa kwa kumkumbuka marehemu mke wake
Wawili hao waliteta na kupelekea Teresa kumwagia maji yaliyochemka.
Wawili hao Gregory na Bi Gilbertson walikutana miaka 7 iliyopita baada ya kifo cha mpenzi mke wake wa mika 30, Maureen.
Lakini kilichozua ubishi na hatimaye janga ilikuwa ni wazo tu ambayo Bi Teresia anasema aliona kama hapendwi tena na akaamua bora waachane iwapo Bwana Gregory ataendelea kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake wa zamani japo ni marehemu.
Wawili hao walipooana miaka 7 iliyopita
Gilbertson aliondoka kwenda kupika chai lakini akarejea akiwa amefoka na bakuli la maji moto ambayo alimwagia mumewe kichwani kutoka nyuma.
Bi Teresa sasa anakabiliwa na mashtaka ya kusababisha maumivu na uchungu mwingi kwa mumewe ambaye amemtaliki.
Gilbertson atahukumiwa tarehe 24 Machi.

No comments:

Post a Comment