Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 18 March 2015

KLINIKI KWA NJIA YA SIMU YALETA MAFANIKIO NZEGA

Importance Of Mobile Phones
Na Hastin Liumba, Nzega
HUDUMA za kliniki ya afya ya uzazi kwa akinamama wajawazito walio na maambukizi ya VVU na wasio na maambukizi umeanza kuonyesha mafanikio hospitali, zahanati na vituo vya afya wilayani Nzega mkoani Tabora.



Huduma hiyo maarufu kwa jina la ‘MOBY’ inayotumika kusajili akinamama wajawazito na kutunza taarifa zao, imekuwa msaada mkubwa kwa watoa huduma za afya ya uzazi.

Hayo yalielezwa kufuatia ziara Mratibu wa Mawasiliano wa shirika lisilo la kiserikali la EGPAF ambao ndiyo watoaji wa vifaa ikiwemo simu hizo chini ya ufadhili wa CDC na USAID nchini Mercy Nyanda

Mratibu wa huduma za afya ya uzazi kwa mama na mtoto wilayani Nzega Tausi Kibonge alisema huduma ya simu inatumika kwa baadhi ya zahanati na vituo vya afya na imerahisisha zoezi la utoaji huduma kwa akinamama wajawazito kwa kuwa mteja anapata huduma stahiki.

‘Huduma hii ni nzuri taarifa za wateja zinatunzwa kwenye simu na kwenye vitabu pia, ukisahau kumpa mteja huduma fulani simu inakukumbusha, pia inatupunguzia gharama za ufuatiliaji kwani Muuguzi mmoja tu anaweza kuwahudumia ikiwemo kuwatumia meseji za kuja kliniki’, aliongeza.

Akielezea faida na mafanikio wanayopata kwa kutumia huduma hiyo Muuguzi wa Zahanati ya Mwanhala  Mwanaidi Rashid Msumbiji alisema tangu waanze kutumia huduma hiyo mwezi Juni 2014 mwitikio wa akinamama kuhudhuria kliniki umeongezeka.

 Naye Muuguzi wa Zahanati ya Samora  Hilda Mussa alisema tangu waanze kutumia huduma hiyo ufanisi wa kuwahudumia akinama wajawazito umeongezeka kwani simu zinakulazimisha kumhudumia kila kitu anachostahili.

‘Kama kuna mteja fulani hajaja kliniki simu inakukumbusha ili uwataarifu watoa huduma za majumbani (HBC) au WAJA wamfuatilie ili afike kliniki kupata huduma kama anavyostahili’, alieleza.

Wakielezea changamoto kadhaa walizobaini katika huduma hiyo, watoa huduma hao walisema kitendo cha kujaza taarifa za wateja kwenye simu na kwenye vitabu vya pembeni kinampa kazi mbili kwa wakati mmoja Muuguzi, ni bora kujaza sehemu moja tu.

Walisema simu hizo pia zinakata kukubali taarifa za wajawazito wenye mimba zaidi ya 5 aidha kwa maeneo ya vijijini walieleza kuwa mtandao huwa unasumbua, suala ambalo walisema linafanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment