Mabaki ya majengo yaliyokuwa hifadhi ya kaburi la rais Saddam Hussein
Wanajeshi wa Iraq na wapiganaji wanaopigana na wanamgambo wa Islamic State karibu na mji wa Tikrti wanasema kuwa kaburi na la rais wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein karibu limeharibiwa kabisa.
Picha za shirika la habari za AP zilionyesha mabaki ya kaburi hilo lililojengwa kwa njia ya kifahari lililo katika kijiji cha al-Awja.
Aidha zinaonesha picha za Saddam zikiwa zimeondolewa na mahala pake kuwekwa picha za viongozi wa wapiganaji ikiwemo picha ya jenerali wa Iran Qassem Soleimani anayewashauru wapiganaji wanaopigana vita na islamic state.
Mwaka uliopita jamii ya wasunni wanaokaa katika eneo hilo liliondoa mwili wa kiongozi huyo wa Iraq ambaye kungolewa kwake madarakani na majeshi ya muungano yaliongozwa na Marekani iliitumbukiza taifa katika vita ambavyo vimechacha hadi leo.
Haijulikani hadi wa leo ulizikwa wapi mwili huo.
Mwandishi wa BBC nchini Iraq anasema kuwa kuna shauku kuwa huenda wapiganaji wa Shia ndio walioharibu kaburi hilo ilikulipiza kisasi cha mateso waliyopita mikononi mwa kundi la Islamic state na wapiganaji wa Sunni.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment