Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 25 March 2015

DIWANI ASHAURI SERIKALI KUWAANGALIA WAKULIMA WA TUMBAKU


Na Hastin Liumba, SikongeDIWANI wa kata ya Mole wilaya ya Sikonge mkoani Tabora  Mbarpuk Omar ameishauri serikali kuangalia namna ya kumsadia mkulima wa zao la Tumbaku kwa kuwarushu wawe na namba binafsi (TB) hata kama mkulima huyo ana Hekari moja.


Ushauri huo aliutoa wakati akifanya mahojiano na mwandishi kuhusu hali halisi ya vyama kadhaa vinavyoeelemewa na madeni na kushindwa kukopesheka Benki.

Diwan huyo alieleza ili mkoa usimame kiuchumi na mkulima aondokane na madeni yanayotokana na mikopo ya pembejeo ni vyema akaruhusiwa kuwa na namba binafsi ili akope pembejeo yeye kama yeye.

Aidha alisema ili hilo lifanikiwe pia anashauri utaratibu ulioposasa wa pembejeo ufutwe na mikopo ya pembejeo yaachiwe makampuni kama ilivyokuwa zamani.

Alisema mfumo wa sasa unambana mkulima wa tumbaku na endapo serikali italiona hili basi itakuwa ni mkombozi kwa mkulima.

Alitoa mfano wa chama msingi cha ushirika ambacho kiko kwenye kata yake ya Mole cha Usangaya ambacho kilikuwa na wanachama zaidi 470 sasa kinakaribia kufa kutokana na kukosa sifa ya kukopesheka kwani kinakabiliwa na madeni makubwa.

Alisema chama hicho kina madeni makubwa ya msimu wa kilimo wa 2013/2014 kutokana na wakulima wasio waaminifu ambao walitorosha tumbaku kutokana baadhi ya kauli tata za kauze popote.

Diwani huyo alisema endapo mkulima ataruhusiwa kulima kwa namba binafsi itasaidia wakulima wasio waaminifu kujulikana.

Tayari mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wa wakulima wa tumbaku kanda ya magharibi (WETCU) Mkandala Gabriel Mkandala ameanza kuchukua hatu kunusuru vyma 69 kati ya vyama 202 vilivyokosa sifa ya kukopesheka Benki.

Mkandala alisema wameanza kutoa pia mafunzo ya namna viongozi wa vyama vya msingi vya ushiria vitakavyofanya kazi zao na kuepusha migongano na madeni.

No comments:

Post a Comment