
Bobby Christina Brown (kulia)
Mwana wa aliyekuwa mwanamuziki wa 'rhythm n blues' marehemu Whitney Houston, Bobby Christina Brown ameondoshwa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory na sasa yuko katika nyumba ya kurekebishia tabia katika Jimbo la Atlanta, lakini uhamisho huo sio ishara kwamba hali yake inaimarika.
Bobby Christina alihamishwa hadi katika kituo hicho siku ya Alhamisi baada ya madaktari wa hospitali ya Emory kujaribu tena kuona iwapo anaweza kupumua bila kutumia mashine.
Hata hivyo, hakuweza kupumua na inadaiwa kuwa madaktari wanasema bado hajapata fahamu.
Bobby Brown na Pat Houston walisaidia katika kubeba mizigo ya Bobby Christina kutoka hospitali hiyo hadi kituo hicho cha kurekebishia tabia ambacho kinadaiwa kuwa kizuri katika uangalizi wa wagonjwa wa muda mrefu.
Inadaiwa kuwa Bobby Brown ambaye ni babaake Bobby Christina ana imani kwamba mwanawe atapata fahamu.
CREDIT: BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment