Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage
Na Jacquiline Mrisho -
MAELEZO, Dodoma
Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wamefanikiwa
kuhamasisha baadhi ya wawekezaji kuwekeza katika sekta ya dawa ya binadamu na
vifaa tiba ili kupunguza uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi.
Hayo
yamesemwa leo mjini Dodoma na Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Charles Mwijage
alipokuwa akijibu swali la Mhe. Khadija Ali (Viti Maalum) aliyehitaji kufahamu
mpango wa Serikali wa kutumia malighafi zilizopo kuzalisha baadhi ya dawa na
vifaa tiba.
Waziri
Mwijage amesema kuwa Serikali inaendelea na Mkakati Unganishi wa Maendeleo ya
Viwanda (IIDS) pamoja na Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Miaka Mitano ambayo ambayo
yote inalenga kuondoa changamoto ya kununua dawa na vifaa tiba kutoka nje ya
nchi.
“Serikali
kupitia mashirika yake ya MSD, TIRDO, NHIF, TIB na TFDA wamepewa jukumu la
kuandaa mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya dawa za
binadamu pamoja na vifaa tiba kwa hiyo kupitia wizara yangu na TIC tayari
tumefanikiwa kuwahamasisha wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani”, alisema
Mwijage.
Baadhi
ya wawekezaji hao kuwa ni JSN Solution ambao watajenga kiwanda cha kuzalisha IV
Fluid, China Dalian International Economic Development Group Co. Ltd ambao watajenga
kiwanda cha kutengeneza vifaa tiba, Zinga Pharmaceuticals Ltd pamoja na Hainan
Hualon ambao watatengeneza madawa mbalimbali ya binadamu.
Waziri
Mwijage amesema kuwa kupitia Ubalozi wa Korea nchini, Kampuni ya Boryung
Pharmaceuticals Co. Ltd itatengeneza madawa ya Penicilin Orals Solids
Antibiotics, wakati Agakhan Foundation Network watazalisha dawa mbalimbali.
Waziri
Mwijage ameongeza kuwa kujengwa kwa viwanda vya dawa za binadamu na vifaa tiba
kutakuwa na fursa pana ya kuwahakikishia Watanzania nafasi za ajira kwa vijana
nchini kipindi kifupi kijacho.
No comments:
Post a Comment