Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wajumbe wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye
ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta wakimsikiliza Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye
ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
wataalamu wa masuala ya gesi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya
kufungua mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi
wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Wazalishaji Petroli Afrika,
Mhandisi Mahaman Laouan Gaya mara baada ya kufungua mkutano wa masuala ya soko
la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
Salaam
............................................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali itaendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha rasilimali ya gesi na
mafuta inakuwa ni chachu ya kukuza uchumi wa taifa na wa wananchi kwa ujumla.
Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan amesema hayo leo 22-Nov-2016
Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa mwaka wa kujadili masuala
ya gesi na mafuta barani Afrika ulioandaliwa na Kampuni ya Getenergy ya
Uingereza.
Katika hotuba yake, Makamu
wa Rais amewahakikishia washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania imeweka
mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi na itakuwa bega
kwa bega na wadau wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha
uwekezaji utakaofanyika unakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.
Amesisitiza kuwa kwa sasa Serikali
ya Tanzania inaendelea na mkakati kabambe
wa kusomesha wataalamu wa fani ya mafuta na gesi ndani na nje ya nchi ili
kuhakikisha taifa linajitosheleza kwa wataalamu hao ambao watakuwa na uwezo na
ujuzi wa kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa katika sekta za gesi na mafuta.
Makamu wa Rais amesema
Tanzania imegundua kiasi kikubwa na gesi na ana imani kubwa kuwa mafuta nayo yanapatikana
hivyo ni muhimu kwa mataifa ya Afrika kujipanga
kuwa na wataalamu wake wazalendo wa kutosha watakaoshikiri katika uchumi wa
gesi na mafuta kwa kuajiriwa kwenye makampuni yanajihusisha na utafiti na
uchimbaji wa gesi na mafuta.
Makamu wa Rais Samia Suluhu
Hassan amesema anaimani kubwa kuwa rasilimali ya gesi na mafuta zitakagundulika
na kuchimbwa barani Afrika zitasaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa
mataifa hayo, uchumi ambao utasaidia kuimarisha utoaji wa huduma bora za kijamii
kwa wananchi katika nchi husika.
Mkutano huo wa siku Mbili wa
Kimataifa umekutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya gesi na mafuta kutoka ndani
na nje ya nchi ambao wanajadili kwa kina na kubadilishana uzoefu kuhusu njia
bora za uwekezaji katika sekta hiyo barani Afrika.
Kwa upande wake,Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesisitiza kwa Serikali itaendelea
kusomesha wataalamu wake ndani na nje ya nchi ili kujitosheleza kwa wataalamu
wa sekta hiyo.
No comments:
Post a Comment