Mkaguzi wa Ndani Mkuu
wa Serikali Msaidizi Stanslaus Mpembe akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
kuhusu zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara ya Fedha na
Mipango, mkoani Dodoma.
Katibu wa Chama cha Wastaafu wa Mkoa wa Dodoma John Kanyeto
akielezea jinsi zoezi la uhakiki
lilivyoeshendwa mkoani Dodoma.
Mstaafu Christina Mashamba (kushoto), akifanyiwa uhakiki na
Wakaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Mmanispaa ya Dodoma, kushoto ni Jestina
Naftaz na kulia ni Devotha Masanja.
Wastaafu mbalimbali wakiwa kwenye foleni kusubiri zamu yao
ya kuhakikiwa jijini Dodoma.
Wastaafu wakipeana maelekezo
wakisubiri kuitwa kuhakikiwa mkoani Dodoma
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Wizara
ya Fedha na Mipango, imezindua zoezi la uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa pensheni
na Wizara hiyo. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa
ya Dodoma mkoani Dodoma.
Lengo la kufanyika kwa zoezi hili ni kuhuisha
orodha ya malipo ya Wastaafu kwa mara ya mwisho zoezi hilo lilifanyika mwaka
2014.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Mkaguzi wa
Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Stanslaus Mpembe, alisema kuwa zoezi hilo
litafanyika kwa muda wa siku tano katika Kanda ya Kati ambayo imejumuisha mikoa
mitatu ya Morogoro, Dodoma na Singida.
Mpembe
alisema lengo la kufanyika kwa zoezi hilo ni kubaini mabadiliko ya taarifa za
Wastaafu kama vile kufariki ili kuepuka kulipa Wasiostahili.
‘Zoezi
hili linafanyika kutokana na utaratibu uliojiwekea Wizara kufanya uhakiki wa
Wastaafu baada ya muda fulani, zoezi hili litafanyika nchi nzima. Mpembe
alisema’
Aliongeza
kuwa zoezi hilo litaisaidia Serikali kuhakikisha Wastaafu wote wanapata haki
zao na kwa wakati.
Aidha
alitoa wito kwa Wastaafu kujitokeza kwa wingi kuhakikiwa ili waweze kupata haki
zao za msingi, bila kusahau viambatanisho wanavyotakiwa kuwa navyo ili
kurahisisha zoezi hilo.
Naye
Katibu wa Chama Cha Wastaafu wa Mkoa wa Dodoma John Kanyeto aliishukuru
Serikali kwa kuwajali na kukubali ombi lao kuhusani Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Ashatu Kijaji kwa kufikisha
ombi lao walipofanya nae kikao la kulipwa mafao yao kila mwezi badala ya kila
baada ya miezi mitatu.
‘Niwaombe
Wastaafu wenzangu wajitokeze kwa wingi kwani zoezi hilo ni la kwa faida yao.
Kanyeto aliongeza’.
Kwa
upande wa mstaafu Bi. Halima Matonya alisema kuwa zoezi hilo limeenda vizuri na
ameipongeza Serikali kwa kuwajali na kuwakumbuka, na amewapongeza pia Waratibu wa zoezi hilo kwa kujipanga vema
na kutoa maelekezo vizuri hivyo kufanya zoezi hilo kuchukua muda mchache.
Tayari
zoezi kama hilo la uhakiki wa wastaafumwanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na
Mipango limefanyika katika Kanda za Pwani na Nyanda za Juu Kusini ambapo
ilijumlisha mkoa wa Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Katavi, Ruvuma, na Songwe.
Baada
ya kukamilika kwa zoezi hilo kanda ya kati, zoezi hilo litaendelea katika Kanda
ya Kaskazini ambapo litajumuisha Mkoa wa Kilimanjaro,
Arusha, Manyara na Tanga.
No comments:
Post a Comment