Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakazi wa kijiji cha Nsola ambapo alikagua miradi mbali mbali ya ufugaji samaki
ikiwa sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua
shamba la kilimo cha kisasa Greenhouse (Bandakitalu) la Ngongoseke lililopo kijiji cha Nsola wilayani
Magu mkoa wa Mwanza
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza kwa makini mwanafunzi Evodia Anatori wa shule ya sekondari ya kata
ya Idetemya akionyesha kwa vitendo namna ya kuchanganya kemikali kwenye maabara
ya shule hiyo iliyopo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia
wananchi wa Idetemya mara baada ya kufungua bweni la wanafunzi wa kike katika
shule ya sekondari ya kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kumsalimia kwenye maeneo ya Nyakato mkoani Mwanza.
........................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi
mkoa wa Mwanza kuimarisha maradufu doria katika Ziwa Victoria kama hatua ya kukabiliana
na tatizo la uvuvi haramu ambao umepunguza kwa kiasi kikubwa samaki kwenye ziwa
hilo.
Makamu wa
Rais ametoa maagiza hayo katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika wilaya
za Kwimba, Misungwi na Magu mkoani Mwanza katika ziara yake ya kikazi
ambayo imeigia siku ya PILI mkoani humo.
Makamu wa
Rais amewataka viongozi hao kuwachukulia hatua kali za kisheria watu
watakaokamatwa wakivua kwa zana haramu ua kwa sumu ili kukomesha tatizo hilo
katika Ziwa Victoria.
Ameonya
kuwa wavuvi haramu wakiachwa waendelee kufanya uvuvi huo wataharibu ziwa lote
hasa mazalia ya samaki hali ambayo itasababisha viwanda wa kusindika samaki
mkoani humo kufungwa na mamia ya watu kukosa ajira kutokana na shughuli za
uvuvi.
Akizindua
na kuweka mawe ya msingi kweye mabweni ya wanafunzi wasichana katika
shule za sekondari ya Idetemya wilayani Misungwi na shule ya Sekondari ya
Archbishop Anthony Mayala wilayani Kwimba, Makamu wa Rais amepongeza juhudi za
viongozi wa mkoa wa Mwanza na wadau wa maendeleo kwa kujenga mabweni hayo
ambayo yatasaidia wasichana kuondokana na mazingira hatarishi ikiwemo kupata
mimba.
Makamu wa
Rais amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
nchini kuweka mikakati madhubuti ya kujenga mabweni ya wasichana kama hatua ya
kukabiliana na tatizo la wanafunzi kupata mimba na kuacha shule.
Akisalimia
mamia ya wananchi wa maeneo ya Igoma na Nyakato jijini Mwanza waliojitokeza
barabarani ili kumsalimia, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia
wananchi hao kuwa ahadi zote zilizotolewa na viongozi hao wakati wa kampeni
zitatekelezwa ikiwemo tatizo la ajira kwa vijana.
Amewahimiza
wananchi waunge mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kubaini
walarushwa na watendaji wanaohujumu miradi ya maendeleo ili wachukuliwe hatua
za kisheria.
Amesisitiza
kuwa serikali ya awamu ya tano inataka kuona rasilimali zilizopo nchini
zinatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote na sio kwa idadi ya
watu wachache.
Akiwa
mkoani Mwanza Makamu wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan amekagua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya
maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara na
kuwaeleza mipango ya mikakati ya serikali ya awamu ya Tano ya kuwaletea wananchi
hao maendeleo.
Katika
hatua nyingine, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amechangia mabati 100 na
mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi
katika shule ya sekondari ya wasichana ya Archbishop Anthony Mayala wilayani
Kwimba mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment