Mwenyekiti
wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Singida
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiongoza kikao hicho, kushoto kwake ni
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina Mageni Lutambi, wa kwanza
kulia ni Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Lameck Nchemba na anayefuata
ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Mhe. Martha
Mlata.
Mbunge wa Viti maalum CCM Singida Aisharose Matembe akichangia hoja katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Singida (RCC).
Meneja wa SIDO Mkoa wa Singida Shoma Kibende akichangia hoja katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Singida (RCC).
Na Nathaniel Limu-Singida
Wafanyabiashara
wa kuku wa asili/kienyeji mkoani Singida wamejipatia mapato ya zaidi ya
shilingi bilioni 1.8, baada ya kuuza kuku 151,242 katika kipindi cha
mwaka jana hadi sasa.
Hayo
yamesemwa juzi na kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji
Beatus Choaji wakati akitoa taarifa ya uendelezaji wa kuku wa asili,
kwenye kikao cha kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa mjini
hapa.
Chowaji amesema mapato hayo yamepatikana baada ya kuku hao 151,242 kusafirishwa na kuuzwa nje ya mkoa ikiwemo jijini Dar-es-salaam.
“Kuku
wa asili wakifungwa vizuri kwa kudhibiti ugonjwa wa mdondo na
kuzingatia kanuni za ufugaji bora wanaweza kuleta mabadiliko makubwa na
ya haraka ya kipato. Kuku wa asili pia ni lishe bora hususani kwa watoto
na akina mama”, ameongeza Choaji.
Ili
kuimarisha ufugaji kuku wa asili amesema imependekezwa halmashauri zote
zitekeleze mkakati wa kuchanja kuku kwa wakati moja mara tatu kwa mwaka
kwa kutumia watoa chanjo wasiokuwa wataalam wa mifugo.
Akisisitiza
amesema “Mkakati huu unatarajiwa kuanza mara halmashauri
zitakazokamilisha utoaji wa mafunzo kwa watoa chanjo hao. Halmashauri
zimesisitizwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mkakati huo ili kuinua
kipato cha wananchi kwa haraka zaidi”.
Mapema
Mkuu wa Mkoa wa Singida na mwenyekiti wa kikao hicho, Mhandisi Mathew
John Mtigumwe, akifungua kikao hicho ameagiza kuwa wananchi
wahamasishwe, ili wasiendelee kuuza chakula walichovuna msimu uliopita
kiweze kuwafikisha msimu ujao wa mavuno.
Mhandisi
Mitugumwe amesema kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA)
mvua za msimu huu zinatarajiwa kunyesha kwa kiwango cha chini ya
wastani.
“Hivyo
ni jukumu letu sote kuhimiza na kushauri wananchi kufuata kanuni bora
za kilimo na kupanda mazo ya kipaumbele yanayostahimili ukame, na
yanayokomaa mwa muda mfupi.
Wakati
huo huo Mkuu huyo wa mkoa, ametumia fursa hiyo kutoa shukrani zake za
dhati kwa wananchi wadau wa elimu, wafanyabiashara, kampuni za simu za
viganjani na mashirika ya umma na binafsi, kwa kushiriki kutekeleza
agizo la rais Magufuli la kumaliza uhaba wa madawati mashuleni.
No comments:
Post a Comment