Balozi wa India nchini
Tanzania ,Sandeep Arya kushoto akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Thobias Mwilapwa wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa pili
kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena
Saidi.
Balozi wa India nchini
Tanzania ,Sandeep Arya akizungumza wakati wa kongamano hilo kushoto
kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na Waziri wa
Habari
Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye
Balozi wa India nchini
Sandeep Arya kushoto akiteta
jambo na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye katikati wakati wa kongamano la wafanyabiashara kutoka nchini India na Tanga uliofanyika ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
jambo na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye katikati wakati wa kongamano la wafanyabiashara kutoka nchini India na Tanga uliofanyika ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Baadhi ya wafanyabiashara
kutoka nchini India na
Tanga wakimfuatilia hotuba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa wakati akifungua kongamano la wafanyabiashara juzi kwenye ukumbi wa hotel ya Tanga Beach Resort
Tanga wakimfuatilia hotuba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa wakati akifungua kongamano la wafanyabiashara juzi kwenye ukumbi wa hotel ya Tanga Beach Resort
KAIMU
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Thobias Mwilapwa amewakata wawekezaji kutoka
nchini India kuwekeza mkoani hapa kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za
kiuchumi zikiwemo kilimo,utalii,elimu na Afya ili kuweza kunufaika
nazo.
Mwilapwa alitoa kauli
hiyo juzi wakati
akifungua kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na India uliofanyika katika
hotel ya Tanga beach jijini Tanga uliowahusisha wafanyabiashara kutoka India na
Mkoa wa Tanga.
Kongamano hilo lilikuwa na lengo
lilikuwa ni kushirikisha mawazo na kuona ni kwa namna gani wanaweza kuzitumia
fursa mbalimbali zilizopo mkoani hapa ili kufanya uwekezaji ambao utaweza
kuleta tija ya kimaendeleo.
Alisema kuwa India ni
miongoni mwa nchi
ambazo zimesaidia kukuza uchumi kwa baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania hivyo uwepo
wao katika suala la uwekezaji linaweza kuwa chachu ya kuweza kuinua kasi ya
ukuaji wa maendeleo.
“India ni miongoni mwa nchi ambazo zimesaidia kukua kwa uchumi kwa
baadhi ya nchi dunia ikiwemo Tanzania kutokana na hilo niwatake muona namna ya
kuwekeza mkoani hapa kwani yapo maeneo mengine mnayoweza kufanya hivyo
“Alisema.
Awali akizungumza Balozi
wa India nchini,
Sandeep Arya alisema ujio wa Waziri Mkuu wa India Tanzania umeongeza ari kwa
Taifa ilo kuona haja ya kuendelea kuwekeza na kusaidia katika masuala
mbalimbali ya afya, Elimu Bishara na Kilimo.
Alisema kuwa soko la
India linahitaj
bidhaa zenye ubora na rahisi hivyo anaamini kutokana na ushirikiano wa nchi hizi
mbili kufanana mahitaji kutakuwepo na fursa kubwa ya muingiliano wa kibiashara
ambao utaleta tija na faida kwa pande zote mbili.
Hata hivyo alisema licha
kushirikiana
na Tanzania katika miradi mbalimbali ikiwemo ya maji, matibabu ya kansa lakini
wanatoa nafasi 350 za mafunzo nchini india kila mwaka ili kuwapatia nafasi watu
kujifunza jinsi India inavyofanya kazi katika shughuli zake za
uzalishaji.
Naye, Waziri wa Habari,
Utamaduni Sanaa
na Michezo, Nape Nnauye ambaye alikaribishwa kuzungumza alisema moja kati ya
mipango ya Serikali ya awamu ya tano chini Rais John Magufuli ni kuhakikisha
inakuza uchumi na kuleta maendeleo kwa mwananchi wa hali ya nchi hivyo hakuna
haja ya wananchi kukata tamaa.
No comments:
Post a Comment