Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania Dr. Stephen Nindi akichangia jambo wakati wa mkutano huo
Bw.Emanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili(wa pili kulia) akitolea ufafanuzi jambo wakati wa mkutano huo
Bw.
Marcely Madubi kutoka Asasi ya kiraia ya Care International (wa pili
kulia) akichangia jambo katika kipengele cha Changamoto na mapendekezo
kuhusu upangaji , utekelezaji na usimamizi wa mipango na matumizi ya
Ardhi
Bw.
Jamboi Baramayegu kutoka Ujamaa-CORT akichangia jambo juu ya hangamoto
na mapendekezo katika uandaaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya
matumizi ya Ardhi.
Bw.
Gerald Mwakipesile Afisa Mipango wa Tume ya Mipango na Matumizi ya
Ardhi akizungumza juu ya Mpango wa Elimu kwa Umma kuhusu maswala
mbalimbali yanayokabili upangaji,utekelezaji na usimamizi wa matumizi ya
Ardhi nchini.
Mratibu
wa Mradi wa Ardhi yetu kutoka Asasi ya Kiarai ya Care International Bi.
Mary Ndaro akizungumzia jambo juu ya Taasisi zinazojihusisha na Mipango
ya matumizi za Ardhi nchini na kusisitiza ushirikiano.
Bw. Paulo Tarimo ambaye ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo akitolea msisitizo Jambo
Profesa
Aldo Lupala ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi na Mkuu
wa Kitivo cha Usanifu Majengo Akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa
mkutano huo
Mwakilishi kutoka Asasi ya Kiraia ya kimataifa Oxfam Naomi Shadrack akichangia jambo wakati wa Mkutano huo.
Profesa
Aldo Lupala ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi na Mkuu
wa Kitivo cha Usanifu Majengo akipitia kuona kazi zinavyofanyika katika
makundi mbali mbali.
Majadiliano katika Makundi Mbalimbali yakiendelea
Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa
Wadau mbalimbali wa Mashirika ya Kiraia na Sekta binafsi kwa kushirikiana
na TUME ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi wanatarajia
kukabidhi ripoti maalum kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya
Makazi,William Lukuvi ifikapo Desemba mwaka huu ripoti hiyo ikiwa ni ya uandaaji
wa mpango kazi wa utekelezaji wa Makubaliano ya Mkutano mkuu wa Wadau wa
Mipango ya Matumizi ya ardhi nchini .
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa Kikosi kazi uliofanyika
mkoani Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya
Matumizi ya Ardhi, Dk Stephen Nindi alisema vitu muhimu katika nchi
ambavyo vinasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi ni upangaji
wa matumizi bora ya ardhi.
Alitaja vitu ambayo ni miongoni vinavyokwamisha kwenda kwa kasi kwa zoezi la upangaji wa matumizi bora ya ardhi ni pamoja na ufinyu wa bajeti na ukosefu wa teknolojia mpya zinazoweza kupima na kupanga ardhi kwa mwendo wa haraka zaidi.

Aidha Dkt.Nindi alisema Kikosi kazi hicho kilikutana katika mkutano huo
kwa lengo la kuandaa ripoti hiyo ambayo inatarajiwa kumfikia Waziri Mh. Lukuvi
na kuona ni namna gani nchi nzima inafanikiwa kuwa na mpango mzuri wa
matumizi bora ya ardhi na kuondoa migogoro iliyopo sehemu mbalimbali nchini.
Alisema viongozi wa kitaifa wanapaswa kutambua kwamba ardhi ni suala
nyeti na mtambuka hivyo wanapaswa kushiriki kikamilifu katika mipango ya
matumizi bora ya ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa itaweza kusaidia kupunguza
migogoro ya ardhi inayojitokeza.
"Tunatarajia kufikisha ripoti hii kwa Muheshimiwa Waziri Lukuvi na yeye ataona ni namna gani atakavyowashirikisha Mawaziri tofauti tofauti ambao kwa namna moja au nyingine wanaingia katika suala hili la mpango wa matumizi bora ya ardhi ikiwemo katika sekta ya Madini, Kilimo, Misitu na Mifugo na kuona ni namna gani wataweza kutenga bajeti ambayo itaweza kuingia katika suala hili la matumizi bora ya ardhi,"alisema Nditi
Dkt. Nindi aliongeza kuwa ripoti hiyo itawezesha suala la upangaji wa matumizi bora ya ardhi linakuwa suala la kitaifa na kuiwezesha serikali kupanga bajeti itakayofanya mchakato huo wa upimaji na upangaji wa matumizi bora kwenda kwa haraka na kufikia vijiji vingi zaidi.
Naye Mratibu wa Programu ya Mradi ya Ardhi yetu kutoka asasi ya kiraia ya CARE INTERNATIONAL nchini Tanzania, Bi.Mary Ndaro alisema serikali inapaswa kuweka dhamira kisiasa ya kuweka utayari wa kufanya suala la ardhi kuwa ni kipaumbele na kuongeza bajeti ya fedha katika suala la matumizi ya ardhi.
Alisema asasi za kiraia zipo tayari kufanya kazi na serikali pamoja na Wizara zinazohusika na suala la matumizi bora ya ardhi na kuhakikisha mabadiliko yanapatika katika suala hilo
"Tupo tayari kuungana na serikali katika kuhakikisha suala hili linapewa kipaumbe na kupunguza migogoro inayoendelea kujitokeza kwa sasa ya ardhi hivyo sisi tupo tayari kuona serikali inatoa mwongozo wake kupitia Wizara zinazohusiana na masuala ya ardhi kwa pamoja tuungane na kushikamana katika kusaidia suala hili linafanikiwa na vijiji vinapangwa na kupimwa kwa matumizi bora ya ardhi," alisema Ndaro.

Pia Bi. Ndaro alisisitiza wananchi kuwa watulivu na kukwepa muingiliano
kwani asasi hizi zimejizatiti kusaidia wananchi hivyo rai yangu kwa baadhi ya
asasi za kiraia zinazo penda kusaidia mchakato huu ziapaswa kujitokeza kwa
wingi ilikuweza kumaliza shughuli hii kwa haraka zaid kwani tukiiachia serikali
peke yake haitoweza kumaliza sehemu zote kwa wakati kwani inabajeti ambayo ni ndogo
ambayo inaweza kumudu vijiji vitano tu kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment