Mzazi Sakina Lembo |
Na Dotto Mwaibale
MZAZI Sakina Lembo (26) mkazi wa Mbagala Kibonde Maji ambaye alizuiliwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), kutokana na deni la sh. 338,257 baada ya kufanyiwa oparesheni ya uzazi uongozi wa hospitali hiyo umemruhusu kuondoka bila ya masharti yoyote.
Akizungumza wakati akitoka hospitali hapo baada ya kuruhusiwa mama yake na Sakina, Edith Chausa alisema analishukuru gazeti la Jambo Leo kwa kutoa taarifa hiyo ambapo wahusika wameona na kuchukua uamuzi wa kumruhusu binti yake kuondoka hospitali na mtoto wake bila ya masharti yoyote" alisema Chausa.
Alisema kabla ya kuchukua uamuzi wa kwenda kwenye vyombo vya habari waliomba kuondoka na mzazi huyo lakini walikataliwa kwa kuambia mpaka alipe deni hilo ambalo hawakuwa na uwezo wa kulipa.
"Baada ya kutoka taarifa hii kwenye vyombo vya habari amekuja wodini mkurugenzi wa Muhimbili na kuchukua maelezo kwa binti yangu huku akilalamika kuwa mbona hatukusema kama hatukuwa na fedha badala yake tumewashitaki kwenye vyombo vya habari" alisema Chausa.
Chausa alisema binti yake na mtoto waliruhusiwa kuondoka hospitali hapo saa saba mchana na kuwa hali ya mtoto na mama yake inaendelea vizuri.
Chausa ameiomba serikali kuangalia suala zima la wakina mama wanokwenda kujifungua kulipishwa kiasi kikubwa cha fedha kwani wengi wao hawana uwezo huo.
No comments:
Post a Comment