Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya
mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza
na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim
(katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania Dk.
Serafina Mkuwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa
saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha
jijini Mwanza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim kwenye moja ya
mabanda yaliokuwa yanatoa huduma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa
saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha
jijini Mwanza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia
mkono wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa
saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa uzazi kwenye uwanja wa Furahisha
jijini Mwanza.
Sehemu ya Wanawake waliojitokeza kwennye uzinduzi huo.
......................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahakikishia
wananchi kuwa serikali imeweka mipango na mikakati thabiti ya kukabiliana na
idadi kubwa ya vifo vinasababishwa na saratani hasa saratani ya matiti na mlango wa kizazi kote
nchini.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika viwanja vya furahisha jijini
Mwanza wakati akizundua kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na
mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani humo.
Katika
hotuba yake kwa mamia ya wananchi wa mkoa wa Mwanza waliojitokeza katika
uzinduzi huo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ikiwa ni nchi
mojawapo Kusini mwa Jangwa la Sahara ina kiwango cha juu cha vifo vya saratani
ya matiti na mlango wa kizazi ambapo asilimia 60 ya vifo vyote vinavyotokea Kusini mwa jangwa la Sahara
vinasababishwa na saratani hiyo.
Makamu wa
Rais amesema kuwa vifo vingi vinatokana na uelewa mdogo, imani potofu,gharama
kubwa za matibabu,unyanyapaa na kuwepo kwa vituo vichache wa kufanyia
uchunguzi hapa nchini ambapo kwa sasa
tiba ya mionzi inapatikana katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Roas, Dar es
Salaam.
Katika
kukabiliana na tatizo hilo, Makamu wa Rais amesema kuwa Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imepokea kiasi cha shilingi
bilioni Tano kutoka Benki ya Dunia fedha ambazo zitawezesha vituo Vitatu kwa
kila Halmashauri ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za uchunguzi na matibabu
ya mapema ili wanawake kote nchini hasa wale wale wa vijijini waweze kupata
huduma hizo kwa urahisi na kwa ukaribu kwenye maeneo wanayoishi.
“Wote ni mashuhuda kwa namna saratani
ya mlango wa kizazi inavyosababisha vifo vingi hali ambayo hutokana na magonjwa wanaogundulika na ugonjwa kuwa
tayari wamefikia hatua isiyotibika na kwa pamoja saratani hizi mbili
husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akinamama”
Makamu wa
Rais amesisitiza kuwa kwa sasa tayari kuna vituo takribani 300 vinavyotoa huduma
za upimaji wa dalili za awali katika vituo vya afya kote nchini na hivyo vituo
vipya vitaongeza huduma endelevu ili kupunguza vifo vitokanavyo na saratani.
Makamu wa
Rais pia ametoa wito maalum kwa wanaume kote nchi kuunga mkono kampeni hiyo kwa
kuwaruhusu wanawake na wasichana kwenda kupima saratani hiyo na amewapongeza na
kuwashukuru wanaume wa mkoa wa Mwanza kwa kuwasindika wake zao na watoto wao wa
kike kwenda kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kupima saratani hiyo na kupatiwa
tiba.
Makamu wa
Rais amepongeza Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania- MEWATA na wadau wote kwa
kuanda zoezi la huduma za uchunguzi wa dalili za awali za saratani ya mlango wa
kizazi.
Kwa upande
wake, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa
nchi zenye wagonjwa wengi wa saratani ya mlango wa kizazi na pia ndiyo
inaongoza katika nchi za Afrika mashariki.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
No comments:
Post a Comment