Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa kuelekea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala
katika bara la Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akifuatilia kwa makini hotuba mbali mbali kabla hajahutubia hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika
unaojadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala
katika bara la Afrika
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama
ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia
na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, mjini Arusha.
Rais wa Mahakama ya Afrika Mhe. Jaji Justice Sylvain Ore akihutubia
wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama
ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia
na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
Wajumbe wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama
ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia
na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
Wajumbe wakipewa jarida la Mahakama ya Afrika mara baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada kuhutubia Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama
ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia
na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
.......................................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya
Tanzania imepiga hatua kubwa katika kulinda na kutetea haki za binadamu kwa
kuzingatia maazimio mbalimbali ya ndani ya nchi na ya kimataifa ikiwemo haki ya
kuishi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Arusha kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati anafungua
mkutano wa mazungumzo wa masuala ya demokrasia na haki za binadamu ya Mahakama
ya Afrika ya Watu na Haki za binadamu.
Amesema
Tanzania ni mfano wa kuigwa barani Afrika kwa kuzingatia na kutekeleza ipasavyo
mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolenga kuhakikisha wananchi wake wanapata
huduma bora na za msingi ikiwemo huduma ya afya na elimu bila kubaguliwa
kutokana na ulemavu,jinsia,rangi au dini.
Amesisitiza
kuwa Serikali itaendelea kutekeleza na kuzingatia matamko mbalimbali ya Dunia
yanayolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii ikiwemo haki
ya kuishi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kufurahishwa na hatua zinazochukuliwa na baadhi
ya nchi za Afrika katika kulinda na kutetea haki za binadamu hasa haki za
wanawake na kusema kuwa bado kuna umuhimu mkubwa kwa nchi ambazo zinazosuasua
kutekeleza mikataba hiyo kufanya hivyo ili kuhakikisha wanawake na watoto
wanapata haki sawa katika jamii.
Katika hatua
nyingine, Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa
katika kuingiza wanawake katika ngazi za maamuzi na kwa sasa mpango kabambe unafanyiwa
kazi ili kuhakikisha sekta binafsi ambayo bado inaidadi ndogo ya wanawake
kwenye ngazi za maamuzi kufanya hivyo na kwamba tafiti mbalimbali zilizofanyika
nchini zinaonyesha kuwa wanawake wengi walioingizwa kwenye bodi mbalimbali bodi
hizo kwa sasa zimeongeza ufanisi wa kazi maradufu.
Kwa upande
wake, Rais wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu Justice Sylvain
Ore amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwani unalenga kujadili na kuweka
mikakati inayolenga kuhakikisha nchi za Afrika zinazingatia na kulinda haki za
bindamu hasa haki za wanawake kwa kiwango kikubwa.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
No comments:
Post a Comment