Katikati ni
Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala
za mikoa
na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo akitembelea shule ya
Sekondari
Pangani wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Pangani,Zainabu Issa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso
mwenye suti nyuma
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Naibu Waziri wa Tamisemi akiwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Pangani wakati wa ziara yake leo. |
Serikali ipo kwenye mpango
wa kuanza utekelezaji wa ujenzi wa vituo
vya afya katika kila kata nchi mzima ili kumaliza changamoto ya upungufu huo
uliopo kwa sasa katika maeneo mengi.
Rai hiyo imetolewa na Naibu
Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa
na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo hapo Jana wakati wa ziara yake
wilayani Pangani.
Alisema kuwa mpango huo
unatarajiwa kuanza utekelezaji wake kuanzia mwaka
ujao wa fedha kwa kila Halimashauri kujengewa kituo kimoja cha afya katika
ngazi yakata .
Alisema kuwa kupitia mpango huo serikali itaweza kwa kiasi fulani kufikia
lengo la lake iliyojiwekea la kila kata kuwa na kituo cha afya ili kusogeza
huduma karibu na wananchi.
Aidha Naibu Waziri huyo
alisema kuwa licha ya utekelezaji wa Sera ya afya
kutiliwa mkazo katika maeneo mengi hapa nchini bado mpaka sasa Tanzania
mzima inavituo vya afya 440 pekee.
Kwa Upande wake Mkuu wa
Wilaya yaPangani Zainab Abdallah alisema kuwa
wilaya hiyo inakata 14 lakini ina kituo cha afya kimoja hali inayosababisha
changamoto ya utoaji wa huduma.
"Wilaya yetu maeneo kata
nyingine zimetenganishwa na mto Pangani
hivyo kutoka na hali hiyo tumelazimika kujenga kituo cha afya katika kata za
ngambo ili tuweze kuwahudumia wananchi wote" alisema Dc
huyo.
No comments:
Post a Comment