Mwenyekiti
wa timu ya Bunge,William Ngereja
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza akizungumzia
maandalizi ya timu ya Bunge kuelekea mashindano ya Afrika Mashariki
yatakayofanyika nchini Kenya.
Mkurugenzi
wa Benchi la Ufundi la
timu ya Bunge,Stephen Ngony’ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu
akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye hotel ya Tanga Beach
Resort ambapo timu ya Bunge imeweka kambi.
Mwenyekiti
wa timu ya Bunge,William Ngereja
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza katika akiteta
jambo na wachezaji wa timu ya Bunge kushoto aliyevaa tisheti nyekundu ni
Mkurugenzi wa
Benchi la Ufundi la
timu ya Bunge,Stephen Ngony’ani alimaarufu Proffesa Maji
Marefu
TIMU ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “Bunge
Sports Club”imetua mkoani Tanga leo kuweka kambi ya siku tatu kwa ajili ya
kujiandaa na Mashindano ya Bunge la Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza
kutimua vumbi Desemba 14 mwaka huu mjini Mombasa nchini
Kenya.
Kikosi cha timu ya Bunge kilichosheheni wachezaji wa
michezo ya mpira wa miguu,wavu,riadhaa ,kuvuta kamba na mchezo wa gofu ambao
inajumuisha wachezaji 60 ambao watashiriki kwenye mashindanio hayo
yanayotazamiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila kuonekana kujipanga
imara.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga
mara baada ya timu hiyo kutua,Mwenyekiti wa timu ya Bunge,William Ngereja
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza alisema kuwa maandalizi
kwa upande wa timu yao yamekamilika kwa asilimia
kubwa.
Alisema kutokana na umuhimu wa mashindano hayo
waliamua kuweka kambi mkoani Tanga ili kuendana na hali ya hewa kabla ya kwenda
nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ikiwa ni mpango wa
kuimarisha kikosi chao.
“Mimi nisema
tu sisi kama timu ya Bunge nia na lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunaibuka na
ushindi kwenye mashindano hayo na ndio maana tumeamua kuweka kambi mkoani Tanga
lakini pia hata hivyo pia kikosi chetu kimeimarika kutokana na usajili ambao
tumekuwa tukiufanya kila baada ya miaka mitano “Alisema
Ngeleja.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la
timu ya Bunge,Stephen Ngony’ani alimaarufu Proffesa Maji Marefu alisema kuwa
kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo
huo.
Alisema timu hiyo ipo kwenye mazingira mazuri ya
kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mashindano hayo ili kuweza kutimiza
dhamira yao waliojiwekea ya kutwaa
ubingwa.
Kwa upande wake,Nahodha wa timu ya Mpira wa Pete ya
Bunge,Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kawe alisema kuwa wamejiandaa
vizuri kuhakikisha wanafanya vizuri ili kutimiza dhamira waliojiwekea ya kuibuka
na Ubingwa.
No comments:
Post a Comment