Mkuu wa Kitengo
cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA), Sarah Kibonde Msika, akikabidhi mifuko 100 ya saruji kwa Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha Vijijini, Bw. Wambura Yamo kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya Shule za Msingi za wilaya hiyo, hivi karibuni.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha Vijijini, Bw.Wambura Yamo, akimshukuru Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ally Masaniga baada ya kukabidhiwa mifuko 100 ya saruji na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia), kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya Shule za Msingi za wilaya hiyo.
Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha Vijijini, Bw. Wambura Yamo, akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia), mara baada ya kumkabidhi mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya Shule za Msingi za wilaya hiyo.
Sehemu ya mifuko 100 ya saruji iliyotolewa msaada na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya Shule za Msingi za wilaya hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia), Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha Vijijini, Bw. Wambura Yamo (katikati) na Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo, Ally Masaniga wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano hayo, wilayani humo hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia), akiagana na Afisa Mipango wa Wilaya ya Kibaha Vijijini, Bw. Wambura Yamo, mara baada ya makabidhiano hayo, wilayani humo hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment