Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani), kabla ya uzinduzi rasmi wa Bodi ya NIC Jijini Dr es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Laston Msongole (Kushoto), vitendea kazi ikiwemo sheria za masuala ya Bima na miongozo mingine ya sekta hiyo ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Bodi ya Shirika hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) pamoja na viongozi wengine wa Serikali na Maafisa wa Shirika hilo baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Bodi ya Shirika hilo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, akielezea mikakati mipya ya Shirika hilo katika kuboresha utoaji wa huduma za Bima za aina mbalimbali kwa wateja wao, wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Shirika hilo, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango)
Na
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
Waziri wa Fedha na
Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameahidi kushirikiana na Taasisi zote zilizo chini
ya Wizara yake kwa kuhakikisha zinajiendesha kwa faida ili Serikali ifaidike na
mapato yatokanayo na biashara za Taasisi na Mashirika yote kwa lengo la kukuza
uchumi wa nchi pamoja na kupunguza umaskini.
Dkt. Mpango
aliyasema hayo katika uzinduzi wa Bodi ya Wajumbe wa Shirika la Bima la Taifa (NIC),
uliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es
Salaam.
Katika uzinduzi huo
Waziri Mpango ameishauri NIC kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi walioko
vijijini na mijini ili watambue umuhimu wa Bima mbalimbali zinazotolewa na
Shirika hilo.
Aliongeza kuwa Shirika
hilo linatakiwa kubuni mikakati mizuri ya kuongeza huduma za bima nchini hasa
katika Sekta ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kwa kuwa sekta hizo zimeajiri idadi
kubwa ya wananchi ililiweze kupata faida na kutoa gawiwo kwa serikali.
“Naishauri Bodi iwe
bunifu na kuhakikisha kuwa huduma za bima zinaelekezwa kwa wananchi waliowengi
vijijini ambao wanakosa huduma hizo kwa kipindi kirefu ili waweze kunufaika na
huduma hizo badala ya kung’ang’ania mijini kama zinavyofanya Benki” alisisitiza
Dkt. Mpango
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, amesema kuwa
Menejimenti itashirikiana bega kwa bega na Bodi iliyozinduliwa ili kurudisha hadhi ya Shirika hilo, lakini
pia itafanya kazi kwa uaminifu na umakini mkubwa ili kuongeza idadi ya wateja
ambao watachangia mapato ya Serikali.
Amesema kuwa
Shirika hilo limejiekeza kupanua wigo wa utoaji wa huduma zake kwa kuanzisha
Bima kwaajili ya wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kuwa eneo hilo halijaweza
kufikiwa na huduma hizo.
Kwa upande wa
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Bw. Laston Msongole, amesema kuwa Bodi hiyo
itahakikisha kuwa shirika hilo linakuwa la kisasa na lenye tija kwa taifa.
Amesema katika
kipindi kifupi cha kulifufua shirika hilo limeweza kupata faida ya zaidi ya
shilingi Bilioni 6.8 hatua iliyoliwezesha kuwalipa wateja wao madai yao ya
bima.
“Katika Kipindi cha
mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya Tano, NIC imewalipa wateja wake madai yao
yanayofikia kiasi cha shilingi Bilioni 1.26 sawa na asilimia 9.8 ya makusanyo
yote ya biashara ya Bima katika kipindi cha Oktoba 2015/2016.
Ameiomba serikali
iridhie maombi ya Shirika hilo ya kuiruhusdu iuze baadhi ya rasilimali zake
yakiwemo majengo na viwanja ili lipate mtaji wa kutosha na kuliwezesha kulipa
madai ya wateja wao ambao wameanza kulitumia tena shirika hilo kwa kasi baada ya
kuboreshwa.
Shirika la Bima la
Taifa (NIC) linashughulika na biashara ya Bima za Maisha na zisizo za maisha,
ikiwemo kuuza bima za mali na ajali ambazo ni Bima za moto, magari, meli,
ndege, wizi na ujenzi hali kadhalika kushughulikia biashara ya soko la pamoja
la mashariki na kusini mwa Afrika (COMESA) na taasisi nyingine za kikanda.
No comments:
Post a Comment