Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, (aliyevaa joho jekundu), akiwa nje ya
Ofisi Kuu ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kilichoko
Changanyikeni Jijini Dar es salaam, wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo hicho
ambapo wahitimu 154 kutoka nchi nane Barani Afrika wametunukiwa Astashahada na
Shahada za Takwimu Rasmi zinazotolewa na chuo hicho.
Na Benny Mwaipaja
MAKAMU
wa Rais Mama SAMIA SULUHU HASSAN, amesema kuwa matumizi sahihi ya takwimu
zilizokusanywa kwa njia ya weledi mkubwa yanaweza kuchochea maendeleo ya
kijamii na kiuchumi kwa kasi zaidi Barani Afrika,
Mama
Samia ametoa kauli hiyo leo wakati akiwatunuku astashada na shahada wahitimu 154 kutoka nchi saba za kiafrika
ikiwemo Tanzania, wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa
Afrika (EASTC) kilichoko Changanyikeni Jijini Dar es salaam.
Amewataka
wahitimu hao kutumia elimu na ujuzi walioupata katika chuo hicho kufanya
utafiti rasmi na wenye viwango ili nchi wanachama walioanzisha chuo hicho
waweze kutumia takwimu sahihi kupanga mipango yao ya maendeleo itakayosaidia
kuwaondolea umasikini wananchi wake
Pause
Mhe. Samia Suluhu Hassan-Makamu wa Rais-Tanzania
Aidha,
amewahakikishia wahitimu kutoka Tanzania waliomaliza masomo yao katika chuo
hicho kwamba serikali itawapatia ajira ili kuongeza kada ya wasomi waliohitimu
mafunzo ya takwimu rasmi ili kuchochea maendeleo ya nchi
Kwa
upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa Tanzania inatekeleza Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa Taifa ambapo moja ya mambo yatakayosaidia kufanikisha mpango huo
ni matumizi ya takwimu rasmi na sahihi na kuwataka wahitimu kutoka Tanzania
kusaidia kufanikisha nchi kuwa nchi ya viwanda.
Pause
Mkuu
wa Chuo hicho kilichoanzishwa miaka 51 iliyopita, Profesa Innocent Ngalinda, ameiomba
serikali ya Tanzania na nchi wanachama walioanzisha Taasisi hiyo ya elimu ya
juu ya Takwimu Rasmi, kuijengea uwezo ikiwemo miundombinu ya majengo pamoja na
wakufunzi ili kiweze kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu hiyo muhimu
Pause
Akitoa
neno la shukurani kwa mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa
Dkt. Albina Chuwa, amesema serikali imejipanga kutumia wataalamu wa takwimu
Rasmi waliobobea walioko serikalini na katika sekta binafsi kufanikisha utafiti
wa sekta ya viwanda unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Pause
Wahitimu
wa Mahafali ya Pili katika Chuo hicho cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wametoka
katika nchi za Nigeria, Ghana, Ethiopia, Somalia, Uganda, Liberia, Rwanda na
wenyeji Tanzania.
No comments:
Post a Comment