Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wananchi wa Nyamagana kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa machinjio ya
Nyakato.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata
maelezo ya ujenzi wa machinjio ya Nyamagana kutoka kwa Mhandisi wa jiji
la Mwanza Ndugu Ezekiel Kunyalanyala (kushoto) kabla ya kuweka jiwe la msingi
la ujenzi wa machinjio ya Nyakato.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka
jiwe la msingi la ufunguzi wa Jengo la Utawala Manispaa ya Ilemela .
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akikikabidhi madawati kwa Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ambayo
yalitolewa na Ofisi ya Bunge ambapo zaidi ya madawati 1074 yalikabidhiwa kwa
wilaya ya Nyamagana na Ilemela.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kufungua jengo la Manispaa ya Ilemela.
..............................................................................................
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muda wa mwezi
Mwezi Moja kuanzia leo tarehe 18-Nov-2016 kwa watendaji na viongozi waandamizi
wa wilaya ya Ilemela wahamie kwenye wilaya hiyo haraka iwezekanavyo na waache
tabia ya kukaa kwenye wilaya nyingine kwa kisingizio cha kukosa nyumba za
serikali.
Makamu wa
Rais ametoa agizo hilo katika hotuba yake kwa wananachi na watendaji wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi jengo
la utawala la Manispaa hiyo na kukabidhi madawati 1,074 yaliyotolewa na ofisi
ya Bunge.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na tabia hiyo na amewataka viongozi
hao wahamie karibu na maeneo yao ya kazi kabla ya muda aliotoa kwisha ili waweze
kuwa karibu na wananchi katika kuwasaidia kutatua kero na matatizo yanayowakabili
kwa haraka.
Akiwa katika
wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wakati anaweka jiwe la msingi katika mradi wa
ukarabati wa mchinjio ya Nyakato jijini Mwanza, Makamu wa Rais ameuagiza
uongozi jiji la Mwanza kusimamia kikamilifu mradi wa ukarabati wa
machinjio ya Nyakato na watendaji
watakaobainika kuhujumu mradi ambao utagharimu zaidi ya shilingi bilioni Tatu
wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Makamu wa
Rais ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwa wananchi na watendaji wa jiji la
Mwanza waliohudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati wa
machinjio ya Nyakato unaohusisha uboreshaji wa jengo la machinjio,tanki la
kuhifadhi maji,ujenzi wa vyumba vya baridi vya kuhifadhi nyama na ujenzi wa
mtambo wa kutibu majitaka yanayotoka kwenye machinjio hiyo.
Makamu wa
Rais katika hotuba yake, amesema hategemei hata kidogo ukarabati wa machinjio
hiyo ufanyike chini ya kiwango kwa sababu ni mradi wa kibiashara ambao
ukikamilika na kuanza kufanya kazi utasaidia jiji la Mwanza kupata mapato
yatakayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.
Makamu wa
Rais pia amemwagiza Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ahakikishe anasimamia
uundaji wa menejimenti ya machinjio hiyo ambayo itafanya kazi vizuri na sio
kuingiza watu ambao hawana uwezo ambao watakwamisha utendaji kazi wa machinjio
hiyo.
Kuhusu
ukusanyaji wa kodi, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza watendaji wa
Halmashauri zote za mkoa wa Mwanza waongeze kasi ya ukusanyaji wa mapato ya
serikali kwa njia ya kielekroniki kutoka kwenye vyanzo mbalimbali fedha ambazo
zitasaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi mkoani humo.
Makamu wa
Rais pia ametoa wito maalum kwa wananchi nchini wahakikishe wanadai risiti
wanaponunua bidhaa mbalimbali kwani kufanya hiyo watasaidia kuongeza mapato
yake ambao yataelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.
Katika
Mkutano wake wa Majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya Siku Tano mkoani Mwanza
na viongozi wa mkoa wa Mwanza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewasisitiza
viongozi na watendaji wa mkoa wa Mwanza wafanye kazi kwa bidii katika
kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za umma.
Ameonya kuwa
serikali ya awamu ya Tano haitasika kuwachukulia hatua kali viongozi na watendaji
ambao watakwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma kwenye maeneo yao ya
kazi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa mkoa wa Mwanza kusimamia
kikamilifu katika kulinda hali ya amani na Utulivu na wachukue hatua kali kwa watu wanaotaka kuharibu amani ya nchi.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
No comments:
Post a Comment