Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 17 November 2016

KITI CHA UMEYA CHAIVURUGA CHADEMA MBEYA MJINI





Na Mwandishi Wetu, Mbeya.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Wilaya ya Mbeya mjini, kimeingia kwenye mgogoro baina ya viongozi  na madiwani.

Mgogoro huo, ambao unatajwa  kujikita zaidi kwenye maslahi binafsi ya watu, huenda ukakiathiri chama hicho kwa kutengeneza mpasuko, kama uongozi wa juu hautachukua hatua za haraka.

Chanzo cha mgogoro huo,unadaiwa umetokana na viongozi wa chama hicho kujaribu kutengeneza mazingira ya kuwafuta uanachama baadhi ya madiwani kutokana na mienendo ya utendaji kazi wao kutoridhisha.



Inatajwa kuwa chama hicho, hakikuridhishwa na utendaji kazi wa madiwani hao hivyo kuwaandikia barua  yenye kumbu kumbu namba CDM/MBY/11/2016/41 iliyosainiwa na Kaimu Katibu Raphael Mwaitege inayowataka  kuhudhuria mkutano mkuu wa wilaya mbeya mjini.



Pia,Madiwani  wote wametakiwa kutoa  maelezo ni kwa nini hawakuudhulia kikao kilichopita cha tarehe 28/9/2016, kushindwa kushiriki shughuli za kijamii kama vile misiba, kutaja idadi ya vikao vya baraza walivyoshiriki pamoja michango ya kifedha waliyokichangia  chama.



Mratibu wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini(CHADEMA), Franky Mwaisumbe, amesema ofisi baada ya kupokea taarifa hiyo iliunda tume ili kufanya uchunguzi wa madai hayo na kwamba imeanza kufanya kazi  November 14, mwaka huu.



Kazi kubwa itakayofanywa na tume hiyo ni  kuwaita na kuwahoji madiwani wanaotuhumiwa, kuwahoji wananchi juu ya utendaji kazi wa madiwani wao.



Mwenyekiti wa Chadema Wilaya Obadia Mwaipalu alipohojiwa kuhusu mkanganyiko huo, alikana taarifa za chadema Wilaya kuwaandikia madiwani hao barua kwa lengo la kutaka kuwahoji na kwamba hakuna mgogoro ndani ya chama hicho.



Huku hayo yakiendelea kwa upande wa uongozi, baadhi ya madiwani  wameeleza kusikitishwa na hatua za viongozi wa chama ngazi ya Wilaya kujikita katika kutengeneza migogoro ndani ya chama badala ya kuwapa woa nafasi ya kuwatumikia wananchi ambao ndio waliofanikisha kuiweka chadema madarakani na kushika halmashauri.



Wamesema, ni mambo mengi yamekuwa yakifanywa na uongozi wa juu wa Wilaya ambayo yamekuwa hayana ustawi mzuri kwa ndani ya chama.



“Kunaviongozi wamefika mahala, wamekuwa wakidiriki hata kuwatukana kwa kuwarushia matusi ya nguoni madiwani viti maalum  na ukiuliza sababu huioni, ukiacha hilo viongozi hao wamekuwa wakiwashawishi wenyeviti wa serikali za mitaa kufanya maandamano wakitaka Meya ajiuzulu kutokana na kushindwa kushughulikia posho zao,”kilisema chanzo cha habari hii.



Sasa ukiangalia posho za wenyeviti zinahusisana nini na meya…. kwani licha ya suala lao kushughulikiwa na mkurugenzi wa halmashauri lakini bado viongozi hao wameendelea kutengeneza malumbano yasiyokuwa na tija.



Tunafahamu kinachotakiwa hapa ni nafasi ya Umeya na si kingine  lakini ni vema taratibu zikafuatwa kuliko kutengeneza skendo zisizokuwa na maslahi kwa chama na kwa wananchi kwa ujumla.
(JamiiMojaBlog)

No comments:

Post a Comment