Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wanafunzi na wazazi waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipiga makofi ya pongeza mara baada ya zoezi la ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza kukamilika katikati ni Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Geita Mhashamu Flavian Kassala ,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ufunguzi wa mabweni ya wanachuo cha maafisa Tabibu Sengerema mkoani Mwanza.
................................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya
awamu ya Tano itaendelea kujenga na kuimarisha ushirikiano na taasisi za kidini
nchini ili kuhakikisha miradi ya kijamii inayotekelezwa na taasisi hizo inaleta
manufaa makubwa kwa wananchi wa Tanzania.
Makamu wa
Rais ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza kabla ufunguzi wa mabweni ya wanafunzi wa Chuo cha Maafisa Tabibu yaliyojengwa
na Kanisa Katoliki Jimbo la Geita kwa gharama ya shilingi milioni 659.
Makamu wa
Rais amesisitiza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za kidini nchini unaolenga
kuimarisha utoaji wa huduma bora za kijamii na hivyo Serikali inaendelea kudumisha mahusiano
mema yaliyopo kati ya Serikali na taasisi hizo za kidini nchini.
Makamu wa
Rais pia amehimiza taasisi za kidini nchini kutumia vizuri misamaha ya kodi
wanayopewa na Serikali ili kuhakikisha misamaha hiyo inakuwa na manufaa
mazuri kwa jamii na sio vinginevyo.
Kuhusu
uhifadhi wa chakula, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonya vikali tabia ya baadhi ya wananchi kuuza mazao
waliyovuna na baadaye kukabiliwa na uhaba wa chakula na kusema tabia hiyo sio
nzuri na lazima ikomeshwe haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment