Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigullu Lameck Nchemba akiwa katika kikao cha 38 cha bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida.
Meneja
wa TANROADS Mkoani Singida Mhandisi Leonard Kapongo akijibu baadhi ya
hoja katika kikao cha 38 cha bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida.
Wajumbe na wadau mbalimbali wa bodi ya barabara wakichangia hoja katika kikao cha 38 cha bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida na Mwenyekiti wa Bodi ya barabara Mkoani hapa
Mhandisi Mathew John Mtibumwe akiendesha kikao cha 38 cha bodi ya
barabara ya Mkoani hapa, Kulia kwake ni Mwenyekiti wa chama cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Mhe, Martha Mlata.
Na Nathaniel Limu- Singida
Waziri
wa mambo ya ndani Mhe. Mwigullu Lameck Nchemba (mb), ameliagiza jeshi
la polisi nchini,kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria
madereva wanaoacha mawe na matawi ya miti barabarani.
Nchemba
ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iramba mkoani Singida, ametoa agizo
hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha 38 cha bodi ya barabara mkoa
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini
hapa.
Amesema
baadhi ya madereva wa magari na hasa yale makubwa,hutumia mawe kuzuia
magari yao kutembea wakati wakiyafanyia matengenezo ya dharura.
“Wakiisha
maliza kuyafanyia matengenezo magari yao, madereva hao huyaacha
barabarani mawe na matawi ya miti ambayo hutumika kutoa tahadhari kwa
vyombo vingine vya moto. Kitendo hicho kinahatarisha maisha na mali
za watumiaji wengine wa barabara kwa vile yanaweza kusababisha ajali”,
amesema Mwigullu.
Kwa
hali hiyo amesema jeshi la polisi linapaswa kuimarisha mawasiliano ili
waweze kuwathibiti na kuwakamata madereva wanaoacha mawe na matawi ya
miti barabarani.
Katika
hatua nyingine, waziri huyo amesema upo umuhimu mkubwa wa wananchi na
hasa wale wanaoishi kando kando ya barabara kuelimishwa juu ya matumizi
bora ya barabara zinazojengwa kwa fedha nyingi ili waweze kuacha
kupitisha mifugo yao na mikokoteni barabarani.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa bodi ya barabara na Mkuu wa Mkoa wa Singida
Mhandisi Mathew John Mtigumwe ameagiza kuwa fedha zinazotolewa na
serikali na wafadhili mbalimbali wa miradi ya barabara matumizi yake
yasimamiwe kikamilifu, ili zitumike kwa miradi iliyokusudiwa.
“Ujenzi
wa miradi hiyo ya barabara ufanane na thamani halisi ya fedha
zilizotumika. Pia kazi za ujenzi wa barabara za ngazi zote wapewe
wakandarasi bora na wenye uwezo wa kutekeleza miradi ikakamilika kwa
wakati. Nasisitiza kuimarishwa kwa usimamizi na ukaguzi wa mara kwa mara
wa miradi ya barabara ili ziwe za kiwango kinachokusudiwa”,amesema.
Wakati
huo huo, mhandisi Mtigumwe ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa
alikuwa meneja TANROADS mkoa, ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa
TANROADS mkoa wa Singida chini ya meneja wake Mhandisi Leonard Kapongo
kwa kazi nzuri ya usimamizi na ukaguzi uliopelekea miradi ya barabara
kujengwa kwa ubora unaofafana na fedha zilizotumika.
No comments:
Post a Comment