Polisi nchini Australia wanasema kuwa watoto wanane wamepatikana wakiwa wamekufa kwenye nyumba moja katika mji wa Cairns eneo la Queensland kaskazini ya Australia.
Vyombo vya habari vinasema kuwa watoto hao wote kati ya miezi 18 na miaka 15 walikuwa wamedungwa visu.
Polisi wa eneo la Queensland wanasema kuwa waliitwa kwenda kwa nyumba hiyo baada ya ripoti kutolewa kwamba mwanamke alikuwa amejeruhiwa vibaya. Lakini ndani ya nyumba hiyo polisi waligundua maiti za watoto wanane.
Inaaminika kuwa watoto hao walidungwa kisu hadi wakafa. Polisi wanasema kuwa mtoto mdogo zaidi kati ya watoto hao alikuwa na umri wa miezi 18 na mkubwa zaidi alikuwa na miaka 15.
Mwanamume ambaye anakisiwa kuwa na amri wa miaka 30 amepelekwa hospitalini akiwa na majeraha ya kisu. Ndugu mmoja wa familia hiyo aliwaambia polisi kuwa mwanamke hiyo alikuwa mama wa watoto hao
Polisi wanasema kuwa hajakamatwa lakini anawasaidia na uchunguzi. Waziri mkuu wa australia Tony Abbott amekitaja kisa hicho kuwa uhalifu mbaya na pia kuzitaja habari hizo kuwa za kuvunja moyo.
Polisi hawajaweza kuthibitisha ambavyo watoto hao waliuawa hadi pale uchunguzi utakapofanyika.
Wanazungumza na watu kadhaa akiwemo mwanamume aliyeonekana karibu na nyumba hio asubuhi na mapema, ingawa hakuna mtu yeyote amekamatwa.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment