WAMILIKI WA BAA WAIFURAHIA
KAMPENI YA TUTOKE NA SERENGETI
Ni takribani mwezi mmoja sasa tangu kampeni ya miezi
mitatu ianze ambapo mpaka sasa imevutia wateja wengi katika droo za kila wiki.
Wakati kampeni ikielekea kuwa ya aina yake has
katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka, kampuni ya SBL imeweza
kutembelea baa tofauti tofauti ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam na kuongea
na mameneja wa baa na wafanyakazi juu ya kampeni inayoendeleana walikuwa na
maoni yafuatayo.
“kwa kiasi kikubwa promosheni hii imeongeza unywaji
wa bia ya Serengeti Premium Lager katika baa hii. Mauzo ya chupa ya Serengeti
yameongezeka zaidi tofauti na kipindi cha nyuma,” alisema Bwana. Limo- meneja
wa baa ya Hawaii iliyoko Kimara Baruti Dar es salaam. Akieleza juu ya uelewa
wake juu ya promosheni inayoendelea,
Bwana. Limo alisema kwamba “Ninachofahamu ni kwamba baada ya kununua bia ya Serengeti,
unaangalia chini ya kizibo na mteja anaweza pata bia ya bure. Pia Punguzo la Shs. 300 katika kila chupa ya bia, kushinda fedha taslim pamoja na Limo
bajaji ni baadhi ya vitu ambavyo wateja wanaweza kujishindia,” aliongeza.
Kwa upande mwingine Bwana. Kavishe, Meneja wa baa iliyoko
Uhuru Garden-Buguruni alionekana kuwa na uelewa zaidi juu ya promosheni hiyo na
kuongeza kuwa imeongeza mapato kwenye bar yake kutokana na wateja kuiagiza kwa
wingi. Akieleza juu ya uelewa wake juu ya promosheni hiyo, Bwana. Kavishe
alisema “ninachojua ni kwamba, unaponunua bia ya Serengeti angalia chini ya
kizibo na utapata nafasi ya kujishindia bia za bure, bajaji na punguzo la bei
ya bia”.
Baa ya mwisho kutembelewa ilikuwa ni ile ya Kambarage
iliyoko Kihonda Morogoro ambapo kaunta ya baa hiyo ilisheheni bia chapa ya
Serengeti Premium Lager, jambo lililoashiria kwamba eneo hilo linawapenzi wengi
wa bia hiyo.
“Tunajivunia kwamba mshindi wa kwanza wa Tutoke na
Serengeti alitoka katika baa hii. Amekuwa mtumiaji mzuri wa bia ya Serengeti
kutoka katika baa hii mpaka siku anatangazwa mshindi” alisema Bwana. Johnston,
Maneja wa baa hiyo. Kwa mtazamo wake anaamini kwamba ili watu waweze kushinda
wanatakiwa kushiriki mara kwa mara kama alivyofanya Rukia .
Tutoke na Serengeti ni kampeni ya miezi mitatu
ambayo ilizinduliwa rasmi na kampuni ya SBL pamoja na B-Pesa mwezi uliopita na washindi wamekuwa
wakizawadiwa zawadi mbalimbali kila baada ya droo inayofanyika kila wiki SBL- Chang’ombe
chini ya uangalizi wa bodi ya michezo ya
bahati nasibu Tanzania.
Zaidi ya kuwazawadia washindi zawadi mbalimbali kama
vile Limo Bajaj, pesa taslim, bia za bure pamoja na punguzo la bia la shilingi 300,
promosheni hii pia imelenga katika kutangaza utalii wa ndani kwa kuwapeleka
wapendanao katika mbuga mbalimbali za wanyama zilizoko nchini ambapo kampuni ya
SBL hulipia gharama zote kuanzia malazi, chakula, na burudani nyingine katika kipindi chote
mabacho wapenzi hao.
Ili kushiriki katika promosheni hii, mshiriki
anatakiwa awe na umri wa zaidi ya miaka 18, anunue bia ya Serengeti Premium
Lager na aangalie chini ya kizibo ambapo atakuta namba ambazo zinatakiwa
zitumwe kwenda 15317 kwa njia ya ujumbe
mfupi wa maneno. Kadiri mteja anavyoshiriki zaidi, ndivyo anavyojiweka katika nafasi
ya kushinda.
No comments:
Post a Comment