Bi Simone Gbagbo
Abidjan, Ivory
Coast
Bi Gbagbo na
watu wengine 82, akiwemo waziri mkuu wa zamani Gilbert Ake N'Gbo, wameshtakiwa
kwa kuhujumu usalama wa nchi, ukabila na kwa kubuni makundi ya uhalifu.
Rais wa zamani
Laurent Gbagbo, ambaye alikataa kukubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu miaka
minne iliyopita, anasubiri kesi yake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa
kivita (ICC) kutokana na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Zaidi ya watu
3,000 waliuawa katika ghasia hizo baada ya rais huyo wa zamani kukataa
kushindwa katika ya kura ya awamu ya pili.
Bi Gbagbo,
ambaye alikuwa anazuiliwa katika kifungo cha nyumbani kwa miaka mitatu,
ameshtakiwa kwa jaribio la kuhujumu usalama wa taifa hilo.
Aliyekuwa
waziri mkuu Gilbert Ake N'Gbo na kiongozi wa chama cha FPI Affi N'Guessan pia
wamefunguliwa mashtaka na Bi Gbagbo.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment