Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 27 December 2014

WATOTO 87 WAZALIWA MKESHA WA KRISMASI


Watoto 87 wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya Krismas, jijini Dar es Salaam na mkoani Rukwa.

Kati ya watoto hao, 71 walizaliwa katika hospitali za Amana na Temeke, jijini Dar es Salaam na 16 katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Rukwa, iliyopo katika Mji wa Sumbawanga, mkoani Rukwa. 



Muuguzi Mkuu wa zamu wa Hospitali ya Amana, Sista Teresia Akida, alisema katika hospitali hiyo, watoto 52 walizaliwa usiku huo, kati yao wa kiume ni 31 na wa kike 21.

Alisema mama mmoja aliyetambulika kwa jina la Asha Abdallah alijifungua watoto wa kiume watatu, ambao hawajatimiza miezi ya kuzaliwa na hivyo kuhifadhiwa kwenye mashine za watoto.

“Watoto wote waliozaliwa katika mkesha wa krismas wapo katika afya nzuri, tukiacha hao, ambao walizaliwa kabla ya siku zao.

Hata hivyo, wapo mapacha wengine wa kike mmoja na wa kiume, ambao wamezaliwa wakiwa na afya njema na kwa muda sahihi,” alisema Sista Teresia.

Mama aliyejifungua watoto watatu, Asha alisema afya yake ni nzuri isipokuwa ya watoto, ambao walizaliwa kabla ya muda wao kufika na kwamba, wananyonya vizuri.

Katika Hospitali ya Temeke, watoto 19 walizaliwa katika mkesha huo, wa kike wakiwa tisa na wa kiume 10.

Ofisa Muuguzi wa Hospitali hiyo, Grace Rusya, alisema watoto hao wamezaliwa kwa  njia ya kawaida wakiwa na afya njema.

Pia Ofisa Muuguzi na Mkunga wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Rukwa, Fides Nduasinde, alisema wototo nane wa kiume na nane wa kike walizaliwa wakiwa na afya njema, huku kila mmoja akiwa na uzito wa zaidi ya kilo tatu.

Alisema wazazi na watoto wote wana afya njema na walizaliwa kwa njia ya kawaida, isipokuwa mtoto mmoja ndiye aliyezaliwa kwa njia ya upasuaji.
Imeandikwa na Frank Monyo (Dar), Arafa Masingo (Sumbawanga) na Furaha Eliab, Njombe
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment