Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Kenya (KNUT) Wilson Sossion
Nairobi, Kenya
CHAMA cha
Walimu Kenya (KNUT) kimeitisha mgomo nchi nzima wa walimu kuanzia Januari 5,
kikieleza kwamba mazongumzo yao na Tume ya Utumishi wa Walimu kuhusu maslahi
yao hayakuzaa matunda.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Sossion ametoa
notisi ya siku saba kwa Wizara ya Ajira pamoja na TSC kabla ya kuanza rasmi kwa
mgomo huo.
Chama hicho kimewataka wanafunzi wote wa
shule za msingi na sekondari kutokwenda shule kuanzia Januari 5 wakati
watakapoanza mgomo huo.
Chama hicho kimeilaumu Tume ya Mishahara kwa
kukaidi kuboresha mishahara ya walimu pamoja na mazingira yao ya kazi.
Sossion alisema: “Tume ya mishahara haijatengua waraka
wake wa kuongeza posho kwa mawaziri na makatibu wakuu.”
Waraka huo uliongesza posho kwa mawaziri hadi KShs.
200,000 kwa mwezi na kwa makatibu wakuu ni KShs. 150,000 kuanzia Januari Mosi,
2015 waraka ambao chama hicho kilitaka utenguliwe kufikia Jumatano iliyopita.
Sossion aliitaka serikali kujiandaa na mgomo huo wa
walimu nchi nzima na kwamba hawatarudi nyuma.
No comments:
Post a Comment