Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 12 December 2014

WAFUASI CHADEMA WAMPIGA MGOMBEA CCM



JESHI la Polisi mkoani Ruvuma, linawashikilia wafuasi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wote wakazi wa Kata ya Matarawe, Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.

Wafuasi hao wanadaiwa kumpiga Bi. Agatha Komba (CCM), ambaye ni mgombea ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Sabasaba katika Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu ambapo Kamanda wa Polisi mkoani humo, Mihayo Msikhela alisema miongoni mwa watuhumiwa hao ni Thomas Emmanuel (25) ambaye ni mfanyabiashara wa Manispaa ya Songea.

Alisema mtuhumiwa huyo inadaiwa ndiye aliyeanza kurusha matofali mawili kwa mgombea huyo. Wengine ni Omary Hassan (28), Beichoma Ponela (25), Ezekieli Chachaka (22), May Haule (31) na Rashidi Sandari (38), wote wakazi wa Kata ya Matarawe.

“Kutokana na vurugu hizi, tumeanza kuweka ulinzi mkali katika kampeni...tukio hili lilitokea Desemba 9 mwaka huu, saa 10 jioni eneo la Matarawe.

“Inadaiwa mgombea huyu alikuwa akimfuata mgombea mwenzake wa nafasi hiyo ili waweze kwenda kwenye mkutano wa kampeni mtaa wa Sabasaba,” alisema.

Aliongeza kuwa, akiwa njiani alikutana na kundi la wafuasi wa (CHADEMA) wakiwa wamebeba matofali mikononi ambao walimsimamisha na kuanza kumshushia kipigo lakini alikataa kusimama na kuendelea na safari ndipo wafuasi hao walianza kumrushia matofali na kumjeruhi.

Kamanda Msikhela alisema mgombea huyo alijeruhiwa kifuani, kupoteza fahamu na baadaye alikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa.

“Tunaviomba vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huu vifanye kampeni zao kistaarabu kwa amani na utulivu, yeyote ambaye atajihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani atachukuliwa hatua za kisheria,” alisema.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Benedicto Ngaiza, alisema Bi. Komba amelazwa katika wodi namba mbili na hali yake inaendelea vizuri, wakati wowote anaweza kuruhusiwa.

CREDIT: MAJIRA

No comments:

Post a Comment