Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu, Arusha
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limesema linafanyakazi na nchi 20 za Afrika kutengeneza mifumo ya kitaifa ya sayansi, teknolojia kusaidia mataifa hayo kufikia malengo yao ya maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Getachew Engida wakati alipopata nafasi ya kutoa kauli ya shirika lake kwenye mahafali ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia iliyopo Tengeru mjini Arusha.
Alisema shirika lake limejikita zaidi kuhakikisha kwamba inatoa elimu itakayowezesha mabadiliko ya sayansi na hivyo kuwezesha wanaume kwa wake kufanyakazi kama wajasirimali.
“Elimu hiyo ni pamoja na mafunzo ya ukusanyaji takwimu, uimarishaji wa viashiria na ubunifu wa vifaa vya ufuatiliaji na kuimarisha utenegenezaji wa sera kwa kuangalia matukio yaliyothibitishwa,” alisema Naibu Mkurugenzi huyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Taasisi hiyo kushiriki mahafali hayo.
Akizungumza mbele ya wahitimu wa Taasisi hiyo na Rais Jakaya Kikwete alisema kwamba sayansi na teknolojia vina nafasi ya pekee katika jamii na hivyo shirika kama UNESCO inachofanya ni kusaidia kuwapo kwa elimu hiyo.
Alisema sayansi na teknolojia ni msingi wa maendeleo kwani kupitia kuboreka kwa vitu hivyo viwili serikali nyingi zitaweza kukabiliana na umaskini uliokithiri na kupeleka watu wake katika maendeleo na ustawi.
Kiongozi huyo wa Unesco pia alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuwezesha kuwepo kwa Taasisi hiyo ambayo ilibuniwa katika mkutano wa aliyekuwa Rais wa Benki ya Dunia, James Wolfensohn, na Rais Nelson Mandela wa Afrika Kusini mwaka 2001.
Ubunifu huo ulifanyiwa kazi na viongozi wa nchi za Afrika Januari 2005 katika mkutano wao wa Abuja ambapo walikubaliana kuanzisha vyuo vinne vya sayansi na teknolojia kwa jina la Nelson Mandela.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida wakipitia ratiba ya mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru, mjini Arusha.
Alisema sayansi inashikilia majibu ya maswali ya maendeleo ya Bara la Afrika katika kukabili umaskini na kuwa na maendeleo endelevu katika sekta zote na jamii.
Naye Rais Kikwete akihutubia mkusanyiko huo aliwapongeza viongozi wa Taasisi hiyo kwa kuendeleza umaalumu wake.
“Taasisi hii ni sehemu ya mtandao wa vyuo vya Nelson Mandela vya Sayansi na Teknolojia katika Bara la Afrika. Chuo hiki cha Arusha ni mahsusi kwa ajili ya kanda ya Afrika Mashariki. Ndiyo maana Hati Idhini (University Charter) niliyokipa Chuo hiki inaeleza bayana kuwa Chuo hiki kinapaswa kuwa chenye hadhi maalum (special status). Hadhi hii yapaswa pia ionekane katika ubora wa elimu inayotolewa hapa. “ alisema Rais Kikwete.
Alisema ubora wake ni matokeo ya ubora wa wahadhiri wake, programu zake na miundombinu yake.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida akitoa kauli ya shirika lake kwenye mahafali ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia iliyopo Tengeru mjini Arusha. Kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohamed Gharib Bilal na baadhi ya viongozi wa juu wa chuo hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues wakifurahi jambo wakati Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (hayupo pichani) alipokuwa akisoma hotuba yake kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia mwishoni mwa wiki Tengeru jijini Arusha.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Madela, Sayansi na Teknolojia wakitoa burudani kwenye mahafali ya pili ya taasisi hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues wakishuhudia burudani iliyokuwa ikitolewa na wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) akiteta jambo na Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru, jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.
Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika tete-a-tete na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (kaitkati). Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.
Pichani juu na chini ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Gharib Bilal akiwatunuku wahitimu mbalimbali wa shahada za juu za uzamili na uzamivu katika sayansi, teknolojia na tafiti za kisayansi wakati wa mahafali ya pili ya taasisi hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa juma, Tengeru jijini Arusha.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria mahafali hayo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya maprofesa wa taasisi hiyo.
Pichani juu na chini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na kamati ya maandali ya mahafali hayo.
No comments:
Post a Comment