Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Lephy Gembe.
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa, zimesababisha mafuriko katika maeneo ya Manispaa ya Dodoma na kuzua hofu kwa wananchi ya kuibuka magonjwa ya mlipuko kutokana na vinyesi na maji taka kuzagaa ovyo.
Akizungumza na NIPASHE Mwenyekiti wa Mtaa wa Njedengwa Mashariki uliopo Kisasa, Denis Said, alisema kuwa nyumba nyingi za maeneo hayo zimejaa maji na kuzingirwa na mafuriko huku vyoo na makaro, navyo vikifurika na kusababisha vinyesi kuzagaa ovyo ndani na mitaani.
Saidi alisema kuwa wamepeleka malalamiko yao kwa mamlaka zinaozhusika kuhusiana na hali hiyo ya hatari, lakini mpaka sasa hayajapatiwa ufumbuzi na kuzidi kuzua hofu kwa wananchi ya kukumbwa na magonjwa hayo.
“Msimu wa mvua umeanza na hizi ni mvua za pili kunyesha, kumetokea mafuriko haya hatujui zikiendelea tutafanyaje maana maeneo mengi wananchi wanalalamika nyumba zimejaa maji ndani vyoo na makaro ya maji taka yamefurika jambo ambalo linaweza kutusababishia magonjwa ya kuhara, ” alisema.
Alisema mafuriuko hayo yamesababisha makaro ya maji taka na vyoo kufurika na maji yake kusambaa mitaani yakiwa na vinyesi.
Alisema baadhi ya maeneo miundombinu ya barabara yake haijawahi kutengenezwa tangu wajenge makazi yao na kuziba kwa kujaa taka.
Saidi alisema ilikuwa bahati nzuri kwani mvua hizo kubwa zilinyesha juzi alfajiri na wananchi kuanza kujihami kwa kuvunja ukuta wa uzio ili kuruhusu maji kupita lasivyo, kungekuwa na maafa zaidi ya mafuriko.
Alisema kuna baadhi ya maeneo ambayo Serikali ilitengeneza barabara na kuweka lami lakini haikuwekwa mifereji na kusababisha maji kukosa mwelekeo hivyo kuishia kwenye makazi yao.
Alisema miundombinu ya barabara imeharibika hata waliotaka kwenda kwenye nyumba za kuabudu wameshindwa kwenda kutokana na magari kushindwa kupita.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Lephy Gembe alithibitisha mafuriko kuyakumba maeneo mengi na Manispaa hiyo na kuanza kuyatembelea ili kushuhudia athari zake na kufanya tathimini.
Gembe aliyataja maeneo hayo yaliyokumbwa na mafuriko kuwa ni Makulu, Makole, Kisasa West , kisasa North, Area D na Ilazo.
Alisema ameunda timu ya wahandisi wa ujenzi kutoka Ofisi za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) na Manispaa ya Dodoma kuchunguza chanzo cha mafuriko hayo.
Gembe alisema wameamua kuchukua hatu hizo haraka kutokana na kuhofia kuwa huenda mvua zinazonyesha msimu huu zikawa kubwa zaidi na kusababisha madhara zaidi ili waweze kushughulikia janga hilo kwa haraka.
Gembe alisema timu hiyo aliyoiunda kuna baadhi ya eneo ilikopita imebaini kuwa mafuriko yamesababishwa na ubovu wa miundombinu.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment