Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 27 December 2014

HANDENI VIJANA SACCOS YAIOMBA SERIKALI KUONGEZA FEDHA KATIKA MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA

 Viongozi wa Handeni Vijana SACCOS wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipowatembelea kufanya tathmini ya Mkopo waliopewa kutoka Mfuko wa maendeleo ya Vijana.

 Afisa Maendeleo ya  Vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Bw. Mbazi Mfinanga(aliyesimama) akifungua kikao wilayani hapo kilichokuwa kikizungumzia changamoto,mafanikio na maoni mbalimbali waliyopata wana vikundi waliopata mkopo kutoka katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
 Baadhi ya wana vikundi ambao walihudhuria kikao kilichoandaliwa na kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Handeni jana,wana vikundi hao walitoa maoni mbalimbali ikiwemo kuiomba Wizara kuendelea kusaidia Vijana na kuongeza kiasi cha mkopo wanaotoa kutoka katika Mfuko wa maendeleo ya Vijana.
 Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Bi.Caroline Malima akiangalia mbuzi ambao kikundi cha Handeni Arts Group kimewapata kupitia Mfuko wa maendeleo ya Vijana.
 Wajumbe wa Kikosi Kazi cha Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo wakiwa wamebeba mbuzi ambao kikundi cha Handeni Arts Group wanaojiusisha na ufugaji na sanaa wamewapata kupitia mkopo  kutoka Mfuko wa maendleo ya Vijana.

Afisa maendeleo ya Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.Mbazi Mfinanga akiwaeleza jambo wajumbe wa kikosi kazi kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo walipotembelea kikundi cha Vijana Group ambacho kilipata mkopo kutoka katika mfuko wa maendeleo ya Vijana ambapo kikundi hicho hununua mifugo na kuuza na ivyo kujiletea maendeleo.

PICHA ZOTE NA:
Daudi Manongi
Afisa mawasiliano
WHVUM

No comments:

Post a Comment