Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.(Picha zote na Eleuteri Mangi- Arusha).
Na Mwandishi Wetu, Arusha
SERIKALI ya Tanzania imeridhia azimio la arusha kuhusi hifadhi ya jamii nchini Tanzania na kusema litatumika kama dira katika kunemeesha watanzania.
Azimio hilo ambalo limetoka baada ya mkutano wa siku tatu wa wadau mbalimbali wa hifadhi ya jamii kutoka bara la Afrika na mashirika ya kimataifa limeelezwa kuwa msingi mkubwa wa ajenda ya Tanzania kuhakikisha wananchi wake wanahaki sawa katika elimu, afya na mwendelezo wa kiuchumi.
Lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba hifadhi ya jamii inasaidia kuwa na maendeleo endelevu kwa kuangalia maendeleo ya binadamu katika ujumla wake.
Mkutano huo wa siku 3 uliohusisha wataalamu 150 kutoka sekta mbalimbali nchini na barani Afrika wakiwemo watengeneza sera, watafiti na wataalamu wa masuala ya hifadhi.
Ukiwa umewezeshwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na UNICEF, ILO, UNAIDS na taasisi ya utafiti wa sera za uchumi EPRI iliyopo Afrika Kusini (EPRI) , mkutano huo umeelezwa na waziri wa fedha Saada Mkuya Salumkwamba umeweka misingi imara ya kuwa na hifadhi ya jamii endelevu inayojibu mipango ya maendeleo ya taifa.
Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akisoma Azimio la Arusha linalohusu hifadhi ya Jamii, alisema kuwa historia imejirudia ambapo yapata miaka 47 (1967-2014) iliyopita Tanzania ilipitisha Azimio la Arusha lililolenga kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini ambao Baba wa Taifa Mwl. Julius Kmbarage Nyerere aliwaita ni maadui wa taifa.
Kukiwa na wataalamu waliobobea katika mifumo ya hifadhi ya jamii kutoka Afghanistan, Bangladesh, Ethiopia, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe ulifanikiwa kutengeneza hoja zitakazotumika kufanya hifadhi ya jamii Tanzania kuwa endelevu.
Waziri Mkuya alishukuru kwa ushiriki wa mkutano na jinsi ulivyokuwa wazi na jinsi wataalamu walivyoweza kutengeneza azimio ambalo linaenda kuwa msingi katika utengenezaji wa sera na sheria kuhusu hifadhi za jamii nchini Tanzania na afrika kwa ujumla.
Mada kadhaa ziliwasilishwa katika mkutano huo ambazo zilizaa majadiliano yenye manufaa kuhusu mwelekeo wa hifadhi za jamii,utengenezaji wa mifumo ya kuweza kuendelea kuwepo kwa hifadhi ya jamii na umuhimu wa uratibu ndani ya serikali kuu, mitaa na mashirika yanayiotoa huduma za hifadhi ya jamii.
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Jama Gulaid (kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb) wakisikiliza azimio la Arusha linalohusu hifadhi ya jamii wakati wa kufunga kongamano hilo.
Waziri huyo alisema kwamba wakati taifa linaelekea katika uchumi wa gesi utakaofanya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 masuala ya hifadhi ya jamii yatakahakikisha haki katika kugawa keki ya taifa na kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata huduma za elimu, afya, na za kiuchumi kwa haki, kwa kuwa mifumo hiyo pia itatakiw akuchochea ajira na ujasirimali huku ilkilinda afya za wahusika.
Kwa upande wake Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani aliisifu Tanzania kwa kuanza mapema kusimamia masuala ya kinga ya jamii ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii na misaada inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia mpango wake wa kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi.
Aidha, Dkt. Gulaid aliipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika na watu wake licha ya kuwa na vivutio vizuri vya mlima Kilimanjaro, hifadhi ya Serengeti na visiwa vya karafuu.
Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha na aliisifu na kuipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika na watu wake.
“Wimbo huu wa Tanzania tofauti na nyimbo za nchi nyingine ambazo wao wanazungumzia askari, watumwa, watawala wakiwemo Malkia na Wafalme”alisema Dkt. Gulaid.
Dkt. Gulaid aliwahakikishia wajumbe wa mkutano huo kuwa wote wapo salama na wapo kwenye mpango wa hifadhi ya jamii kwa kuwa wametambuliwa na kubarikiwa na wimbo wa taifa wa Tanzania ambapo wajumbe waliimba wimbo huo na kuhitimisha kongamano hilo.
Washiriki wa Kongamano hilo wakiimba wimbo wa Taifa baada ya Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid kutoa ombi kabla ya kumalizika kwa kongamano hilo.
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akisistiza jambo wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitia saini Azimio la Arusha kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii huku viongozi mbalimbali wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa wakishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na washiriki wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha akionesha nakala ya Azimio la Arusha alilosaini kwa niaba ya Serikali.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimpongeza Wazri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum baada ya kusaini Azimio la Arusha kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii (katikati) kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb).
Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (kushoto) akipeana mkono na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb) mara baada ya kusaini azimio hilo huku Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishuhudia tukio hilo.
Baadhi ya wajumbe wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha akifuatilia mada wakati wa kongamano hilo.
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) mara baada ya kumalizika kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment