Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Diwani Athuman.
Watu wanne wanashikiliwa na polisi mkoani Ruvuma, kufuatia mlipuko wa bomu ulisababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi askari polisi wawili.
Bomu hilo linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji, lililipuka siku ya Sikukuu ya Krismas, majira ya saa 1.30 usiku, maeneo ya Majengo Kota.
Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Diwani Athuman, alisema mtu aliyefariki dunia hajafahamika mara moja na askari waliojeruhiwa aliwataja kwa jina moja moja kuwa ni Mselemu na Mariamu ambao walikuwa kwenye doria na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana, alisema baada ya tukio hilo, jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na makachero wa upelelezi kutoka makao makuu ya jeshi hilo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, vinaendelea kuchunguza sababu za mlipuko wa bomu hilo.
Alisema tukio hilo lilitokea eneo hilo wakati askari polisi wakilipita gari dogo lililokuwa limeegeshwa pembeni na kutokea kishindo kikubwa kilichowajeruhi askari hao na kusababisha kifo cha mtu huyo.
Alisema kati ya watuhumiwa wanaodaiwa na kuhusika na tukio hilo, mmoja wao ndiye aliyefariki dunia na waliobaki walijaribu kuuvuta mwili wa mwenzao.
Alisema walipoona askari wakikaribia eneo la tukio, walikimbia na kuuacha mwili huo.
Alisema inavyoonyesha watu hao walikuwa wamelenga kuwalipua polisi lakini ghafla likalipuka na kusababisha kifo cha mmoja wao.
Athuman aliongeza kuwa kuna hisia kuwa hizo ni mbinu za wahalifu kupunguza nguvu za jeshi la polisi kufanya kazi yake ipasavyo katika kulinda usalama wa raia na mali zao.
Hata hivyo, alisema ni mapema mno kuhisi kuwa bomu hilo lililotengenezwa kienyeji kuhusisha na jaribio la kutaka kupora silaha askari na kuahidi kuwa upelelezi unafanyika kubaini chanzo chake.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment