Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 17 December 2014

COASTAL UNION KUJIPIMA NA MWADUI LEO MKWAKWANI



NA MWANDISHI WETU,TANGA
MABINGWA wa soka Tanzania Bara mwaka 1988 Coastal Union “Wagosi wa Kaya” inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Mwadui ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michuano wanayokabiliana nayo.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa leo Jumatano kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani lengo likiwa ni kukipa makali kikosi cha Coastal Union kujiwida na mechi yao ya Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prison itakayochezwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Akizungumza leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa mechi hiyo ni miongoni mwa michezo mbalimbali ya kirafiki wanayocheza ili kuweza kukiimarisha kikosi hicho ambacho msimu huu kimepania kufanya makubwa kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania.
Assenga amesema kuwa timu ya Mwadau ya Shinyanga inatazamiwa kuwasili mkoani hapa Jumanne wiki hii tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na upinzani mkali.
Hata hiyo aliwataka wadau wa soka mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo ikiwemo kuangalia wachezaji ambao wamesajiliwa msimu huu kwa ajili ya michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
Hata hivyo alisema kuwa baada ya kumalizika mechi hiyo wataangalia uwezekano wa kucheza mechi nyengine ya kirafiki kabla ya kutua jijini Mbeya ambapo watakwenda kucheza mechi yao ya Ligi kuu.

No comments:

Post a Comment