Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 17 December 2014

WAUMINI WACHANGA MILIONI 11 KUJENGA KANISA


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
Arusha: WAUMINI wa kanisa la Jesus Healing Gospel Miracle Church lililopo eneo la Matejo jijini hapa wamefanikiwa kuchanga kiasi cha zaidi ya milioni 11 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kanisa ambalo linaendelea. 

Hataivyo kuchangwa kwa fedha hizo kulitokana na maono ya Askofu kiongozi wa kanisa hilo ambaye ni Dustan Mwoleka ambapo waumini hao waliweza kuchanga katika harambee iliyofanyika wiki iliyopita. 
Akiongea na waumini hao mara baada ya kumalizika kwa harambee iliyowashirikisha waumini wa kanisa hilo na wageni kutoka nje ya kanisa hili Askofu Mwoleka alidai kuwa tayari kanisa lake limeshaanza ujenzi na fedha hizo zitasaidia sana kwa ajili ya muendelezo wa ujenzi. 
Mbali na hayo askofu huyo alidai kuwa wakaristo wanapaswa kutambua kuwa wanapotoa katika kazi yoyote ile ya bwana wanapata baraka sana na hivyo wanapaswa kuachana na tabia ya kukwepa michango mbalimbali. 
Alisema, hata kama kanisa likiwa na michango ya kila siku ni lazima wakristo mwajijengee tabia ya kufurai na wala sio tabia ya kuchukia kwani kwa njia ya utoaji ndipo mungu anapokutana na watu. 
“tujifunze katika biblia kuwa waliokuwa watoaji kwa mioyo yao ndiyo walibarikiwa na sisi lazima tuziteke baraka za bwana kwa njia ya utoaji hususani kwenye ujenzi wa majengo ya makanisa yetu;aliongeza Askofu Mwoleka. 
Katika hatua nyingine akiongelea ujenzi huo wa jengo kubwa la kisasa lakanisa askofu Mwoleka alisema kuwa mpaka kukamilika kwa jengo hilo kiasi cha milioni 340 kinahitajika na kwa awamu ya kwanza bado kiasi cfha Milioni 150 nacho kitahitajika. 
Aliwaomba wakristo kutoka katika maeneo mbalimbali hapa nchini nao kuweza kuchangia ujenzi wa jengo hilo ili wafikie malengo ya kuweza kuhubiri injili kwa uraisi zaidi.

No comments:

Post a Comment