Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (kulia)
akimkabidhi Bendera ya Taifa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu
ambaye ndiye kiongozi wa Timu ya Mabalozi wa Tanzania walioanza zoezi la
kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza mlima na kuvutia wageni wengi
zaidi nchini.
Balozi
wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajab pamoja na timu ya mabalozi anayoiongoza
kupanda Mlima Kilimanjaro akinyanyua juu bendera ya taifa pamoja na kushangilia
ikiwa ni ishara ya kuuthamini Mlima Kilimanjaro ambo ni chachu muhimu ya utalii
nchini.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Ibrahim Mussa akitoa maelezo ya Mlima Kilimanjaro kwa
Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru akitoa neno la
ukaribisho kwa Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro. Kulia ni Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa TANAPA Ibrahim Mussa.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akizungumza na
Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi muda mfupi kabla ya kuzindua
safari yao ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza ili kuvutia
watalii wengi nchini.
Baadhi
ya Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi wakisikiliza kwa makini hotuba
zilizokuwa zikitolewa kabla ya uzinduzi rasmi wa zoezi lao la kupanda Mlima
Kilimanjaro kwa lengo la kuutangaza ili uweze kuvutia wageni wengi zaidi
nchini.
Mabalozi
wakiwa tayari kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro katika lango la
Marangu. Kutoka kushoto ni Dk. Batilda Burian; Daniel Njoolay; Aziz Mlima; Joseph Sokoine na Ramadhani Mwinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.
Bernard Membe amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika mataifa
mbalimbali ulimwenguni kuhakikisha kuwa wanatangaza vivutio vya utalii
vilivyopo nchini ikiwa ni njia mojawapo ya kutekeleza diplomasia ya uchumi.
Waziri Membe aliyasema hayo wakati akizindua zoezi la
kupanda Mlima Kilimanjaro linalofanywa na mabalozi mbalimbali wanaoiwakilisha
Tanzania nje ya nchi kwa lengo la kuutangaza Mlima Kilimanjaro ili uweze
kuvutia watalii wengi zaidi.
“Bado idadi ya watalii wanaofika nchini kupanda mlima
hairidhishi na jitihada kubwa zinahitajika kufanywa na mabalozi kuhakikisha
kuwa wanautangaza vema mlima kwa kuwa ni hazina ya pekee tuliyonayo inayopaswa
kuwa kitega uchumi kizuri kwa uchumi wan chi yetu” alisema Membe.
Jumla ya mabalozi 14 wanashiriki zoezi
hili ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka kwa lengo la kuutangaza Mlima
Kilimanjaro. Mabalozi hao ni pamoja na Adadi Rajabu (Zimbabwe); Ramadhani
Mwinyi (Umoja wa Mataifa); John Kijazi (India); Batilda Burian (Kenya); Shamim
Nyanduga (Msumbiji); Grace Mujuma (Zambia); na Patrick Tsere (Malawi).
Wengine ni pamoja na Mbarouk Mbarouk (Saudi
Arabia); Joseph Sokoine (Mkurugenzi Bara la Amerika); Ladislaus Komba (Uganda);
Azizi Mlima (Malaysia); Radhia Msuya (Afrika Kusini); Daniel Ole Njoolay
(Nigeria) na Charles Sanga (Balozi mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii).
No comments:
Post a Comment