Meneja
masoko wa familia ya bia ya Tusker na Pilsner, Anitha Msangi (kushoto) na Mkurugenzi
wa masoko, Bw.Ephraim Mafuru katikati na Meneja ubunifu wa bidhaa zote za
kampuni ya bia ya Serengeti Ms. Attu Mynah wakionyesha chupa mpya ya bia ya
Tusker kwa waandishi wa habari hawapo pichani.
Wafanyakazi
wa kampuni ya bia ya Serengeti wakiwaonyesha waaandishi wa habari , hawapo
pichani, mwonekano mpya ya Bia ya Tusker yenye ujazo wa mlimita 330.
Meneja
masoko-Familia ya bia ya Tusker na Pilsner kampuni ya bia ya Serengeti, Anitha
Msangi akiongea na waandishi wa habari , mara baada ya uzinduzi wa chupa mpya
ya Tusker yenye ujazo wa mililita 330.
Wateja
wa bia ya Tusker Lager kwa mara nyingine wamepewa heshima baada ya kampuni ya Serengeti Breweries kuingiza sokoni
chupa ya bia mpya inayojulikana kama “Tusker ml330”
Chupa hii mpya
imezinduliwa mapema hii leo -Golden Jubilee Tower iliyoko jijini Dar Es Salaam mbele
ya waandishi wa habari, Mkurugenzi Masoko wa SBL Bwana Ephraim Mafuru pamoja na
wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.
Akiongea wakati
wa uzinduzi, Bw. Ephraim Mafuru alisema “Mazingira ya kibiashara ya sasa
yanatulazimu kufikiria zaidi ili kuhakikisha kwamba tunaambatana na uhalisia katika
soko huku tukihakikisha kwamba tunamridhisha mteja wetu katika Nyanja zote”.
Kwa upande
wake, Meneja Masoko wa familia ya Tusker na Pilsner Serengeti
Breweries Ms. Anitha Msangi alisema…
“Ninaamini kwamba ubunifu unainua nia na uhitaji kwa wateja. Hivyo basi matarajio
yangu makubwa ni kwa wateja wetu kuipokea na kuinunua chupa hii mpya kwa
wingi.” Anitha aliongeza kwamba chupa hii ya bia itapatikana na kuuzwa nchi nzima
na tutahakikisha kwamba wateja wote wanaipata bila usumbufu.
Bidhaa
hii mpya ina ujazo wa ml 330 na itauzwa kwa bei ya Shilingi 2,300/= kwa bei ya rejareja.
Uzinduzi wa chupa hii mpya upo katika mtazamo wa kampuni wenye lengo la kwenda sambamba
na hali ya soko.
Tusker
ml330 imeongezeka katika idadi ya vinywaji vilivyozinduliwa na kampuni ya SBL
msimu huu ikilenga kutimiza adhima ya kuingiza bidhaa mpya katika soko la
Tanzania. Bidhaa hizo ni pamoja na:-Serengeti Platinum, Jebel Coconut and
Serengeti Platinum ml330
Uzinduzi
wa Tusker ml 330 umekuja katika msimu wa kampeni ya Tusker FanyaKweli ambayo ina lengo la
kuwahamasisha watanzania kutengeneza maisha ya baadae ambayo wote tutajivunia kwa
vitendo wakati huohuo wakijifunza kupitia watu waliopata mafanikio kupitia yale
waliyokuwa wakiyafanya.
No comments:
Post a Comment