Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 8 September 2015

MIGODI YA SHABA KUFUNGWA ZAMBIA NA CONGO


Taarifa kutoka kwa kampuni kubwa ya uchimba ugodi Glencore imesema kuwa imesitisha uzalishaji wa madini ya shaba katika nchi ya jamhuru ya kidemokrasia ya Congo na Zambia.
Hatua hii imesababisha mtikiso mkubwa katika mataifa hayo mawili .
Aidha wasiwasi umeongezeka kuhusuiana na ukosefu wa kazi.
Mwaandishi wa BBC Mattew Davies amesema hatua ya Glenmore itaathiri takriban robo ya uzalishaji wa shaba katika nchi ya demokrasia ya Congo na Zambia.
Image copyright
Image captionKupunguka kwa kasi ya ukuaji nchini China kumesababisha kushuka kwa mahitaji ya shaba .
Afrika ni wazalishaji wa pili wa vyuma.
Zambia hutegemea asilimia sabini ya mauzo ya nje ya madini ya shaba.
Kampuni hiyo imesema itasitisha uzalishaji katika sehemu ya Mopani, Zambia na Katanga DRC kwa zaidi ya miezi kumi na nane.
Kusitishwa kwa uzalishaji kutapunguza uzalishaji wa tani elfu mia nne itakayosababisha mfumuko wa bei ya shaba.
Kwa hivi sasa uzalishaji umepungua kwa asilimia 40 .
Image copyrightReuters
Image captionZambia hutegemea asilimia sabini ya mauzo ya nje ya madini ya shaba.
Mbali na ukosefu wa kazi, hatua hii pia itapunguza mapato ya kodi na zao la nchi.
Uamuzi wa Glenccore unaweza kusababisha kampuni zingine za ushalishaji wa shaba kufuatwa mkondo huo.
Mgogoro huu umesababishwa maelfu ya maili kutoka Afrika nchini China, ambapo kupunguza kasi ya ukuaji kumesababisha kushuka kwa mahitaji ya shaba .
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment