Kutoka kushoto ni Professor Lloyd Binagi (Manamba), James Binagi, Bi. Luise Binagi, Ghati Isanchu na wanandugu wengine wakiwa katika sherehe ya kifamilia iliyofanyika jana Septemba 24,2015 katika Kijiji cha Kenyamanyori ambapo Professor Binagi aliandaa sherehe hiyo kwa ajili ya kumchinjia mbuzi wa supu shemeji yake aitwae Bi.Nyamhanga Samo.
Na:George GB Pazzo
Kwa kabila la Wakurya sherehe ya kumchinjia mtu mbuzi kwa ajili ya supu huchukuliwa kama heshima kubwa miongoni mwa alieandaa sherehe hiyo na yule alieandaliwa sherehe ambapo ndugu, jamaa, marafiki na majirani hualikwa kwa ajili ya kushiriki pamoja katika sherehe hiyo.
Kushoto ndiye Bi.Nyamhanga Samo ambae sherehe iliandaliwa kwa ajili yake na hapa akiwa pamoja na mke mwenzie wakipata chakula
Kushoto ni Hezekia Binagi (Maina) akipokea Supu kutoka kwa Professor Lloyd Binagi.
Bi. Luise Binagi akimpatia Supu mhusika Mkuu wa sherehe Bi. Nyamhanga Samo
James Binagi (Chacha) akimpatia supu Shemeji yake
Geban Winani akimpatia Supu Bi. Otaigo Mohabe
Bi.Luise Binagi akimpatia Supu Bi.Sophia Binagi
Supu hii huandaliwa kwa ustadi wa hali ya juu ni inafaa kunyweka kwa wazee, mwanawake waliojifungua siku za karibuni au mgonjwa kwa kuwa huufanya mwili kuwa imara zaidi.
Wazee wakipata supu
Tamaduni hii ilikuwepo miaka mingi iliyopita na bado inaendelea kuenziwa na familia nyingi katika kabila la Wakurya
Nyama huchomwa kwa ustadi mzuri pia
Waandaaji wa Nyama
Hapa pia Kichuri huandaliwa
Pia vyakula mbalimbali huandaliwa
Baada ya watu kunywa supu na kula chakula, hufuata zawadi kwa mlengwa wa sherehe ambapo alieandaa sherehe huanza kumtuza zawadi za blanketi, vitenge na pesa yule alieandaliwa sherehe
Mzee Maina akimtuza zawadi ya Kitenge mhusika wa sherehe ambae ni shemeji yake
Mzee Chacha akimtuza zawadi ya Kitenge mhusika wa sherehe ambae ni shemeji yake
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Zawadi zikiendelea kutolewa
Wazee katika picha ya pamoja
Wazee wakibadilishana mawazo baada ya chakula
Baada ya Chakula na kubadilishana mawazo
Wanafamilia
Wanafamilia
Wanafamilia
Wanandugu
Wanafamilia
Wanafamilia
Wanafamilia
Watoto nao hufurahia sherehe za kuchinja supu
Hatimae sherehe ikafikia tamati na Muandaaji wake ambae ni Professor Lloyd Binagi akaingia ndani ya gari na safari ya kurejea nyumbani kwake Bomani Mjini Tarime kutoka Kijijini alikozaliwa Kenyamanyori ambapo sherehe ilifanyikia ikawadia
No comments:
Post a Comment