Mgombea ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas Mtemvu (kulia), akipongezana na mgombea udiwani wa Kata ya Keko, Francis Mtawa baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni viwanja vya Mabembeani Keko jijini Dar es Salaam jana jioni
Mgombea ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas Mtemvu, akihutubia katika mkutano huo wa kampeni. Kulia ni mgombea udiwani wa Kata ya Keko, Francis Mtawa.
Katibu Mwenezi wa Jimbo la Temeke, Ali Kamtande akienda jukwaani kuhutubia.
Wananchi na makada wa CCM wa eneo hilo wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Temeke, Oliva Mwambope (katikati), akielekea jukwaani kuzungumza na wananchi katika mkutano huo.
Mtemvu akielekea jukwaani kuhutubia.
Mgombea udiwani, Francis Mtawa akihutubia.
Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakicheza katika mkutano wa kampeni za ubunge na udiwani uliohutubiwa na Mgombea ubunge wa jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu katika viwanja vya Mabembeani Keko jijini Dar es Salaam jana.
Hapa mgombea Udiwani Francis Mtawa (kulia), akisalimiana na makada wa CCM katika mkutano huo.
Hapa ni picha baada ya mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas Mtemvu amesema amejipanga vizuri kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa miaka mitano mingine iwapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mtemvu alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Mabembeani Keko jijini Dar es Salaam juzi.
"Serikali na chama chetu cha CCM tuna mipango ya maendeleo ya miaka mitano tuliyoindaa tunaomba mtuchague tuweze kuikamalisha" alisema Mtemvu.
Alisema wakazi wa eneo hilo wasiwe na wasiwasi wowote wala kuyumbishwa kwani kunafedha sh. bilioni 120 kutoka benki ya dunia kupitia mradi wa UNDP ambazo zitagaiwa katika kila Kata wilayani Temeke kwa ajili ya shughuli za maendeleo na uboreshaji wa miundombinu na makazi ambapo kwa Keko mgao wao ni sh.bilioni 14.
Mtemvu alisema hivi sasa wamejiandaa kujenga barabara za kiwango cha lami katika mitaa kadhaa ya Keko ambazo zitawekwa taa za sola.
Aliongeza kuwa kwa kipindi ambacho walikuwa katika uongozi wamefanikiwa kujenga miundombinu ya barabara, kuweka taa na kujenga shule za sekondary mbili kati ya hizo zikiwa na kidato cha tano na sita pamoja na kuhimarisha kwa huduma za afya kwa kujenga zahanati jambo ambalo ni la kujivunia.
Mtemvu aliwaomba wananchi hao na makada wa CCM katika nafasi ya urais wampe kura Dk. John Magufuli, Ubiunge wampe yeye na udiwani wampe Francis Mtawa ili mambo yaende sawa.
Mgombea udiwani wa eneo hilo Francis Mtawa aliwaomba wananchi wa eneo hilo kutouza nyumba zao mapema bali wasubiri kukamilika kwa barabara hizo zitakazojengwa kwa kiwango cha lami kwani zitaongeza thamani ya nyumba hizo.
Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Hassan Kitigi alisema changamoto kubwa waliyonayo wakazi wa eneo hilo ni eneo la wazi wanalofanyia mikutano kujaa maji wakati wa mvua hivyo vijana kushindwa kuwa na sehemu ya kufanyia shughuli zao mbalimbali pamoja na michezo.
Alitaja changamoto nyingine kuwa ni miundombinu ya barabara na kujaa maji wakati wa mvua.
No comments:
Post a Comment