Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 29 September 2015

MATOKEO YA CHUONI HAYATAKUSAIDIA KUPATA KAZI

Matokeo ya chuoni hayatakusaidia kupata kazi
Kampuni ya kusaili watu kwa nafasi za kazi Deloitte imebadilisha sera zake ilikuficha majina ya vyuo walikosomea wafanyikazi watarajiwa.
Hii inalenga kuondoa upendeleo na ubaguzi dhid yao kwa misingi ya vyuo walivosoma.
Kuanzia mwaka ujao wanalenga wafanyikazi watarajiwa 1,500 ambao ambao programu zao zitaficha vyuo walikosomea ilikubaini iwapo wanapewa nafasi sawa au wanabaguliwa.
Matarajio yao ni kuwa wafanyikazi watarajiwa watapata nafasi sawa pasi na kubaguliwa eti walisomea vyuo ambavyo havina hadhi ya juu ikilinganishwa na vyengina ama wanapendelewa kwa sababu walisomea katika vyuo vilivyo na hadhi ya juu.
Kwa mfano iwapo mfanyikazi mtarajiwa alipata alama ya BA katika chuo ambacho walipata wastani alama ya DA yaonesha kuwa mfanyikazi huyo angalikuwa katika chuo chenye alama ya wastani BA bila shaka angelizoa alama A.
Majina ya vyuo vikuu walikosomea hayatajumuishwa katika maombi ya kazi.

Image captionMakampuni yaondoa matokeo ya mitiani chuoni kama mojawepo ya vigezo vya kutathmini ubora wa wajiriwa.

Deloitte inasema kuwa mpango huu mpya utawapatia nafasi ya ajira watu wenye uwezo na bidii.
Aidha watu wenye uwezo mdogo watapata fursa ya kujiimarisha kimaisha anasema David Sproul, afisa mkuu mtendaji wa Deloitte nchini Uingereza .
Bwana Sproul anasema watu wenye mitazamo tofauti ni bora kwa ustawi wa kampuni kwa sababu wanaashiria mitazamo ya wateja na umma kwa jumla.
Mabadiliko hayo yanatilia pondo hoja ya waajiri ya kutaka kuweko kwa njia mbadala ya kutathmini ubora wa waajiriwa watarajiwa badala ya kutegemea alama ya chuoni na kutupilia mbali bidii na talanta ya mtu.
Ernst and Young ambayo ni kampuni ya uhasibu pia imeondoa matokeo ya mtiani chuoni kama mojawepo ya vigezo vya kutathmini ubora wa mwajiriwa.
Kampuni nyengine ya PricewaterhouseCoopers ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuchukua mkondo huu.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment