Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa timu 14 kucheza katika viwanja saba nchini, ikiwa ni raundi ya tano ya ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.
Simba SC watakua wenyeji wa Stand United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Azam FC watawakaribisha Coastal Union kwenye uwanja wa Azam Complex – Chamazi jijini Dar es salaam.
Mjini Morogoro vinara wa ligi hiyo Young Africans watakua ugenini kuwakabili wenyeji Mtibwa Sugar ambapo timu zote zikiwa na alama 12 baada ya kucheza michezo minne zikipishana kwa tofauti ya magoli, Wana Lizombe Majimaji FC watakua wenyeji wa Ndanda FC kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Wakata Miwa wa Kagera Sugar watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, African Sports wakiwakaribisha wa Mgambo Shooting uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Tanzania Prisons wakiwa wenyeji wa Mwadui FC katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea siku ya Alhamis kwa mchezo mmoja ambapo Toto Africans watakuwa wenyeji wa Mbeya City katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment