Mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mtoto Joyce Michael akizungumza jambo wakati wa Mdahalo huo
Jastin Moses Mratibu wa mradi wa kuzuia ukatili dhidi ya mtoto kutoka Plan International akichangia mchango wake wakati wa mdahalo huo
Ombeni Ally Mkuu wa Shule ya Sekondari Simbani akifafanua Jambo katika mdahalo huo
Ramadhan Lutambi mgombea udiwani kata ya Kibaha maili Moja kupitia Chadema akisisitiza Jambo
Rosemary Mkonyi mgombea Ubunge kupitia tiketi ya ACT akizungumza Jambo wakati wa mdahalo huo
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wanasikiliza mdahalo huo
Wananchi wakiwa wanafuatilia kwa makini mdahalo huo
Na Mwandishi wetu
Jamii
imetakiwa kuwa karibu zaidi na watoto ili kuhakikisha wanalindwa dhidi
ya ukatili na kuhakikisha wanapata haki zao stahiki. Rai hiyo imetolewa
na wakazi wa Kibaha Mkoani Pwani katika Mdahalo wa Walinde Watoto
uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na
Udiwani.
Kwa upande wake mgombea Ubunge
wa Kibaha vijijini kupitia ACT Wazalendo Dk. Rose Mkonyi alisema kuwa
chama chake kinaangalia ni kwa namna gani watazingatia katika Lishe bora
ya mtoto pamoja na namna gani mtoto atainuliwa Kielimu. Aidha Mgombea
Udiwani wa kata ya maili moja kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
‘CHADEMA’ Ramadhani Lutambi alisema chama chake kitaangalia zaidi afya
ya mtoto na kuhakikisha Bohari ya dawa inakuwa na dawa za kutosha.
Hata
hivyo, Watoto waliohudhuria mdahalo huo waliwataka wagombea kutimiza
ahadi wanazotoa wakati wa Kampeni ili na wao waweze kufikia malengo yao.
Watoto walipendekeza serikali ijayo iangalie namna ya kuwalinda hasa
wanapoelekea mashuleni kwani wamekuwa wakitembea mwendo mrefu kwenda na
kurudi shule ambako wamekuwa wakipata madhara na vishawishi vingi
wanapokuwa njiani.
Aidha watoto pia
waligusia suala la rushwa na kwa namna gani linavyorudisha nyuma
maendeleo yao na kuwaomba wagombea wa ngazi zote katika uchaguzi mkuu wa
mwaka huu kuwa waadilifu ili watoto wapate haki zao.
Mdahalo
huo ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production chini ya Wizara
ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto wakishirikiana na UNICEF uligusa
maeneo kumi muhimu ya uwekezaji kwa watoto ikiwemo kuwekeza kuokoa
maisha ya watoto na wanawake, kuwekeza kwenye lishe bora, kuwekeza
kwenye usafi, udhibiti wa miundombinu ya maji taka na ugavi wa maji
katika shule na kwenye huduma za afya pamoja na kuwekeza katika
kumwendeleza mtoto akiwa bado mdogo.
Mengine
ni pamoja na kuwekeza kwenye elimu bora kwa watoto wote, kuwekeza
katika kuzifanya shule kuwa mahali pa usalama, kuwekeza katika kuwalinda
watoto wachanga na wasichana dhidi ya VVU, kuwekeza katika kupunguza
mimba za utotoni, kuwekeza katika kuwanusuru watoto na vurugu,
udhalilishaji na unyonyaji pamoja na kuwekeza kwa watoto wenye ulemavu.
Vuguvugu
hili la kusambaza ajenda ya watoto kupitia midahalo na wagombea wa
nafasi mbalimbali linaendelea kupita mikoa mbalimbali nchini Tanzania
kwani tunaamini kuwekeza katika maeneo haya ya kipaumbele kunaweza
kupunguza umasikini na kuwezesha kuwepo kwa taifa linalostawi na la
usawa.
Unaweza
kusikiliza kipindi cha redio cha Walinde Watoto mahali popote kupitia
redio shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi
kuanzia saa nane mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org na
No comments:
Post a Comment