Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 29 September 2015

NG'OMBE WAWEKWA 'REFLECTOR' ZIMBABWE

Ng'ombe Zimbabwe
Wakazi wanasema kamba hizo zitawawezesha madereva kuwaona mifugo hao kutoka mbali
Wakazi wa wilaya moja nchini Zimbabwe wamevumbua njia ya kuzuia ajali za barabarani zinazohusisha ng’ombe wanaoranda randa.

Wamekuwa wakiwaweka kamba au vitambaa vinavyoakisi mwanga shingoni au kwenye mikia.
Wakazi hao wa wilaya ya Gutu, mkoa wa Masvingo wanasema hilo litakuwa likiwawezesha waendeshaji magari kuwatambua ng’ombe hao kutoka mbali.
Ng’ombe wengi walitoweka kwenye mashamba baada ya Wazungu wengi kufurushwa kutoka kwa mashamba yao mwaka 2000 kufuatia agizo la Rais Mugabe. Wengi wao wamekuwa wakizurura zurura bila wa kuwatunza. Mashamba mengi pia yalibaki bila ua.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment