Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo
Chama cha ACT-Wazalendo, kimedai kwamba baadhi ya wagombea wake wa ubunge, wamekuwa wakitishiwa maisha sehemu mbalimbali nchini.
Kutokana na hali hiyo chama hicho kimewataka wanasiasa kufanya siasa kwa njia ya amani.“Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya watu wamekuwa wakiwaandama wagombea wa Chama jimbo la Chilonwa mkoani Dodoma na Itilima mkoani Simiyu na kuwatishia kuwadhuru iwapo wataendelea na harakati zao za kisiasa mpaka kufikia Oktoba 25 siku ya uchaguzi,” kilidai chama hicho katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa Habari wa chama hicho, Abdallah Khamis. Taarifa hiyo ilifafanua kuwa katika Jimbo la Chilonwa mkoani Dodoma, mgombea wa ACT-Wazalendo, Eva Mpagama, amekuwa akisumbuliwa mara kwa mara na wapinzani wake kisiasa hata kumtishia maisha yake.
“Taarifa hizo za kutishwa kwa Mpagama zimeshafikishwa kwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na kwamba Jeshi la Polisi linafuatilia nyendo za watu wanaodaiwa kumtishia Mpagama juu ya usalama wake,” ilisema taarifa hiyo.
Ilisema tangu Mpagama alipoanza kampeni zake za kuwania ubunge na kubadili upepo wa kisiasa katika Jimbo la Chilonwa, amejikuta anapata maadui wengi na wengine kufikia hatua ya kumtishia maisha. “Wanasiasa tufanye siasa, tuache hulka zisizofaa.
Wanaomtishia maisha Eva Mpagana, wanajijua, sisi tunawajua na mwenyewe ameshawaripoti kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.
OCD wa Chamwino anajua hili….Sisi kichama tunalifanyia kazi kitaalam kwa sababu linahusu eneo la sheria, hivyo wanasheria wetu wanashughulikia,” ilisema taarifa hiyo. Iliongeza kuwa vitisho hivyo kwa wagombea wao kutoka kwa wapinzani wao wa kisiasa, ni baada ya kujua ni hatari kwao kwenye siasa za kistaarabu.
“Kama wangekuwa hawana hofu naye kwenye uwanja huru wa kampeni, wasingemtishia maisha,” ilisema. Aliwataka wananchi kuwakataa wagombea wenye kutumia mbinu chafu kudhoofisha wapinzani wao.
Kuhusu mgombea wa Jimbo la Itilima, Issack Nyasilu, taarifa ilisema tayari taarifa za kutishwa na hatimaye kuharibiwa kwa gari lake la kampeni, zimesharipotiwa katika Kituo cha Polisi Bariadi na kufunguliwa jalada namba BAR/RB/2729/2015.
Alisema taarifa hizo za kutishwa kwa Nyasilu zilifikishwa kituoni kabla ya gari lake kuharibiwa na baada ya kutoa taarifa hizo muda mfupi baadaye gari likaharibiwa na watu wasiojulikana.
Taarifa ya ACT-Wazalendo ilisema kama wanasiasa wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi wanataka kuwaongoza wananchi, hawapaswi kuwatishia wapinzani wao na badala yake wajikite kujenga hoja za kuwashawishi wananchi wawachague wa Chama Chilonwa mkoani Dodoma na Itilima mkoani Simiyu na kuwatishia kuwadhuru iwapo wataendelea na harakati zao za kisiasa mpaka kufikia Oktoba 25 siku ya uchaguzi.
SOURCE: NIPASHE
No comments:
Post a Comment