Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akihutubia wakati wa Ufunguzi wa
mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika
(SARPCCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu ambaye amekabidhiwa Uenyekiti wa
Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) akipeana
mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Msumbiji Dos Santos JANE (kushoto)
ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo mara baada ya kukabidhiana
Uenyekiti katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha
Makamu
wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimpa mkono wa pongezi Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini Ernest Mangu mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa SARPCCO
kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni akihutubia kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za kusini mwa Afrika.
..........................................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Bara la
Afrika kuweka mipango na mikakati madhubuti ya kukabiliana na vitendo
mbalimbali vya uhalifu vinavyotokea katika ukanda huo kama hatua ya kuhakikisha
wananchi wanafanya kazi zao kwa amani na utulivu.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli
hiyo 16-Sep-2016 wakati anafungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi
Kusini mwa Afrika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini
Arusha.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa anaimani kubwa kuwa
mkutano huo utakuwa ni chachu katika kuibua changamoto mbalimbali za kihalifu
na kuzifanyia kazi ipasavyo kwa manufaa ya ukanda huo.
Amesema ni wajibu wa wakuu hao wa majeshi ya polisi
ya kusini mwa Afrika kujiepusha na malalamiko yasiyo ya msingi kutoka kwa raia
ambayo yanasababishwa na vitendo vya urasimu, uzembe na rushwa ili kujenga
uwazi na uwajibikaji.
Makamu wa Rais pia amehimiza kudumishwa kwa
ushirikiano miongoni mwa wakuu wa majeshi ya polisi kusini mwa Afrika katika
kubadilishana mbinu bora za kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa kuvuka
mipaka.
Katika mkutano huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
–IGP- Ernest Mangu amekabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Majeshi ya
Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Nchi
ya Msumbiji Dos Santos JANE.
Shirikisho la SARPCCO lilianzishwa mwaka 1995 kwa
lengo la kuimarisha ushirikiano wa majeshi ya polisi kusini mwa Afrika katika
kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika ukanda huo.
Shirikisho hilo linaundwa na nchi wanachama 15
ambapo baadhi ya nchi hizo ni Angola, Botswana, Msumbiji, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo- DCR-,Malawi, Zambia, Zimbabwe, Madagascar,Swaziland,
Afrika Kusini,Lesotho, Syshelles na Tanzania ambayo ni mwenyekiti mpya wa
SARPCCO.
Tanzania imekabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO wakati
ndio Mwenyekiti mpya wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika inayojulikana kwa jina la (SADC
TROIKA).
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
No comments:
Post a Comment