Hatimaye Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania limezinduliwa Rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Hassan Kamanta aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo na kuoneshwa na ITV kila siku (kuanzia 27/09/2016 - 17/10/2016) saa 12.30 jioni, Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha Enguiki, wilaya ya Monduli mkoani Arusha na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mwakilishi wa DED, DAS, wazee wa kimila, wenyeji wa kijiji cha Enguiki, wafanyakazi wa shirika la Oxfam.
Jumla ya washiriki 15 kutoka mikoa 15 Tanzania wapo katika kijiji cha Enguiki ambapo wataishi katika nyumba za wenyeji wao kwa muda wa siku 21 huku wakifanya shughuli mbalimbali na kujifunza na mwisho mshindi atakayepatikana atajinyakulia zawadi ya vifaa vya Kilimo vyenye Thamani ya Tsh 25,000,000.
Washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula ni pamoja na Lucina Sylivester Assey (Shinyanga), Anjela Chogsasi Mswete (Iringa), Mwanaidi Alli Abdalla (Mjini Magharibi), Marta Massesa Nyalama (Kaskazini Unguja), Christina Machumu (Mara), Betty W. Nyange (Morogoro), Mary Ramadhani Mwiru (Kilimanjaro), Maria Alfred Mbuya (Mbeya), Neema Gilbeth Uhagile (Njombe), Mwajibu Hasani Binamu (Mtwara), Eva Hiprisoni Sikaponda (Songwe), Hidaya Saidi Musa (Tanga), Monica Charles Mduwile (Dodoma), Mary Christopher Lyatuu (Arusha), Loyce Daudi Mazengo (Singida)
Wanakikundi
cha burudani wakicheza na kuimba nyimbo za asili wakati wa sherehe za ufunguzi
wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula uliofanyika katika kijiji cha Enguiki.
Mkuu
wa wilaya ya Monduli, Idd
Hassan Kimanta(kushoto) akipokelewa na Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster(wa tatu kutoka kulia) wakati wa sherehe za
ufunguzi wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula uliofanyika katika kijiji cha
Enguiki.
Wenyeji
wa kijiji cha Enguiki wakihudhuria sherehe za ufunguzi wa shindano la Mama
Shujaa wa Chakula uliofanyika katika kijiji cha Enguiki.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Enguiki, akiwakaribisha wageni katika kijiji chake.
Mkuu
wa wilaya ya Monduli, Idd Hassan Kimanta(wa pili kulia)
akisikiliza baadhi ya faida zinazotokana na shughuli za uzalishaji chakula
zinazofanywa na washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
Mkurugenzi
Mkazi wa shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster akizungumza wakati wa sherehe za
ufunguzi wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula uliofanyika katika kijiji cha
Enguiki.
Washiriki
wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakiimba wimbo wakati wa sherehe za
ufunguzi wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula uliofanyika katika kijiji cha
Enguiki.
Mtangazaji
wa kipindi cha Mama Shujaa wa Chakula ambaye pia ni balozi wa Oxfam, Muigizaji
Jacob Stephen ‘JB’ akizungumza wakati wa ufunguzi wa shindano la Mama Shujaa wa
Chakula uliofanyika katika kijiji cha Enguiki.
Ufunguzi
wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ulihudhuriwa na watu mbalimbali
Mwenyekiti wa kijiji cha Enguiki akiwakabidhi washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula katika familia za wenyeji wao watakapoishi kwa muda wa siku 21.
Kwa taarifa zaidi tembelea www.facebook.com/MamaShujaa
Kwa taarifa zaidi tembelea www.facebook.com/MamaShujaa
No comments:
Post a Comment